tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,121
Hakika bara letu la Africa hatukosi vituko!!
Kuna taarifa zinasambaa mitandaon kumhusu rais museveni. Tangu aingie mstuni mpaka kutwaa kiti cha urais alifahamika kama mtu aliye zaliwa mwa 1943. Na kwa wanaofatilia siasa za Uganda watakumbuka rais huyo wakati anaingia madarakani alisimamia utaratibu wa kubadilisha utawala kila baada ya miaka mitano mitano kwa vipindi viwili yaan miaka kumi.
Mara hamadi miaka kumi sii mingi hiyo hapo!! Daa akapindua katiba akajiongezea muda wa kutawala. Hata ule aliojiongezea akakukuta huo umefika . Kwa wakati huu kuwaridhisha Waganda akaweka ukomo wa urais kuwa ni miaka 75. Huku akijua ni mbali sana kwa yeye kufikisha miaka 75. Mara Hamadi miaka 75 iko mlangoni!
Hapa akapeleka hoja bungeni kutaka katiba ibadilishwe kusiwe na ukomo wa umri wa kuwa rais. Hapo kidoogo wabunge wamemdindia. Kapiga hesabu kaona aje na hii hapa. Kwamba yeye hakuzaliwa mwaka wa 1943 kumbukumbu za kuzaliwa kwake hazikutunzwa vizuri!! Bali alizaliwa mwaka wa 1947.
Cha kujifunza hapa ni kwamba kuwa kutawala kutamu tusifikilie itakua rahisi kuwatoa CCM!
Watatunga kila sheria kuhakikisha wanabaki madarakani. Na swala la kuweka tume huru hili tusahau. Labda tupange kuandamana kama zimbabwe