Rais Museveni: Sijakuwa mgonjwa kwa miaka 31

Rais Museveni: Sijakuwa mgonjwa kwa miaka 31

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
_97150475_f391a643-e3f4-4c69-92da-58480363798e.jpg

Rais Yoweri Museveni

Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafanya kupata matibabu nchini Uingereza mwaka huu.

Lakini sasa rais wa miaka mingi wa Uganda Yoweri Museveni, amenukuliwa akisema kuwa hajawai kuwa mgonjwa kwa miaka 31.

"Mshasikia kuwa Museveni amekuwa mgonjwa au amelazwa hospitalini kwa miaka 31 iliyipota?" aliuliza Museveni.

"Hii ni kwa sababu ninafuata taratibu za kiafya ambazo zimenisaidia kuizuia baaadhi ya magonjwa kama haya, mengi ya magonjwa hata yanazuiwa."

Baadhi ya marais ambao pia wamesafiri ng'ambo kupata matibabu tangu mwaka uliopita ni pamoja na marais wa Angola, Zimbabwe, Benin na Algeria.

Rais wa Zimbabwe ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 amekosolewa na wapinzani kwa kuiongoza nchi "kutoka hospitalini" baada ya kufanya ziara ya tatu nchini humo kupata matibabu mwaka huu.


Chanzo: BBC
 
Sasa mtu kila siku ana dokta! Anyway wacha akufuru Mungu.

Cairo's
 
Museven atakuwa anatuficha....huwezi kaa miaka yote hiyo hujaumwa hata...hasa kwa nchi za kiafrika.........
 
Dah! Kuna watu wana bahati sana. Yani mie katika siku 365 za mwaka, effectively nakuwaga mzima siku hizo 65. Zilizobaki 300 huwa nakuwaga kwenye afya ya kuunga unga...
 
Back
Top Bottom