KWELI Rais Mwai Kibaki aliwaambia waandishi wa habari kuwa ana mke mmoja tu

KWELI Rais Mwai Kibaki aliwaambia waandishi wa habari kuwa ana mke mmoja tu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau wa JamiiCheck.com alihitaji kujua uhalisia wa Kipande cha video kinachomuonesha aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki akizungumza na vyombo vya habari kwamba ana mke mmoja tu kama ni cha kweli au kimetengenezwa.

1726142817667.png



 
Tunachokijua
Mwai kibaki alikuwa Rais wa awamu ya tatu nchini Kenya ambaye alihudumu kati ya mwaka 2002 hadi 2013 na alifariki April 2022, mkewe alifahamika kwa jina Lucy Kibaki ambaye aliyefariki April 2016.

Vyombo vya habari nchini Kenya Kipindi cha utawala wa Rais Mwai Kibaki vilikuwa vikimuhusisha Rais Kibaki kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine tofauti na mkewe Lucy Kibaki na hivyo kupelekea Rais Kibaki kuitisha mkutano wa waandishi wa habari tarehe 03/04/2009 ili kukanusha tuhuma hizo kama ilivyochapishwa na tovuti ya The Guardian tarehe 04/04/2009.

Ambapo baada ya tukio hilo video hiyo ilisambaa na inaendelea kusambaa mpaka hii leo ambapo watu mbalimbali wameendelea kuisambaza video hiyo katika mitandao yao ya kijamii mfano hapa, hapa na hapa

Uhalisia wa video upoje?
Kwa kupitia utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia Google Reverse Image na TinEye umebaini kuwa video ni halisi na wala haijatengenezwa ambapo kituo cha televisheni cha Citizen cha nchini Kenya mwaka 2016 kilichapisha video katika mtandao wake wa youtube ikielezea historia ya Mama Lucy Kibaki ambapo pamoja na mambo mengine kwanza ilianza kuelezea Machi 03 2009 namna ambavyo Lucy Kibaki alitambulishwa kama mke pekee wa Hayati Mwai Kibaki na kukana madai ya kuwa na zaidi ya mke mmoja.

Vilevile kituo cha televisheni cha NTV Kenya kilichapisha video halisi ikihusu suala hilo mnamo Aprili 24, 2022.

Pia, kwenye tovuti ya Nairobi News(NN) Ilichapisha taarifa hii kwenye ukurasa wake mnamo 22 Aprili 2022
1725690147268-png.3089289
Ni kweli..mke wa kibaki alikua moto balaa..mtata mnoo...chek youtube zipo pia..
 
Back
Top Bottom