Rais Mwinyi akutana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho Oman

Rais Mwinyi akutana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho Oman

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1696949363521.png

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi amekutana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman, Jamal al-Moosawi na ujumbe wake Ikulu Zanzibar leo tarehe 10 Oktoba 2023.

Rais Mwinyi amemkaribisha Jamal al-Moosawi Zanzibar katika kile kilichotajwa kuwa ni fursa za kuendeleza ushirikiano katika nyanja tofauti za kihistoria, uhifadhi wa mali kale na kwamba Serikali iko tayari kutoa ushirikiano.

Pia mazungumzo yao wamegusia fursa mbalimbali za uhifadhi wa mali kale katika kubadilishana uzoefu, elimu pamoja na mafunzo ya kujenga uwezo.

Jamal al-Moosawi yuko nchini kujionea historia na uhifadhi wa mali kale na makumbusho Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman.
 
Back
Top Bottom