Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi, leo Septemba 05, amezungumza na wanahabari kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwemo Ripoti ya CAG ya Mwaka 2021.
RAIS MWINYI: NAANZA ZIARA ZA KUSHTUKIZA TAASISI ZA UMMA
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameahidi kuanza kufanya ziara za kushtukiza katika Taasisi mbalimbali za umma.
Amesema lengo ni kurudisha nidhamu katika taasisi za umma na kuhakikisha kila mtumishi anawajibika ipasavyo kwenye majukumu yake.
ZANZIBAR: RAIS MWINYI KUIUNDA UPYA MAMLAKA YA KUZUIA RUSHWA
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa Zanzibar (ZAECA) inatarajiwa kufanyiwa maboresho upya ili kuifanya kuwa na makali Zaidi.
Maamuzi hayo yanafikiwa baada ya kushindwa kuchukua hatua kuhusu Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar iliyobainisha upotevu mkubwa wa fedha za Serikali.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amesema pia ataweka mfumo mipya ili uwe endelevu na kutomtegemea mtu mmoja.
Rais Mwinyi amesema “Tutaijenga kwa watendaji wapya na ninawahakikishia fedha zote zilizopotea watu watawajibika, pia mabadiliko haya yatagusa taasisi nyingine zikiwepo ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mahakama.”
RAIS MWINYI: TUNACHUNGUZA MADAI YA VIJANA WA ZANZIBAR KUONDOKA BILA TAARIFA
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amesema madai kuwa kuna baadhi ya vijana wa Zanzibar wanaondoka Nchini katika mazingira tata na kudaiwa wanaenda kujiunga katika vikundi vinavyodhaniwa kuwa ni vya ugaidi, wanazo na kinachofuata ni uchunguzi.
Amesema “Tumesikia taarifa hizo, hivyo kuhusu ni vijana wangapi, wamekwenda wapi na kufanya nini ili Serikali iweze kuchukua hatua stahiki hilo linafanyiwa kazi.
Ameongeza kuwa “Nimeagiza Serikali ikipata taarifa sahihi kuhusu jambo hilo tutatoa taarifa, lakini tuwe macho ili kuhakikisha jambo hilo halifanyiki kwa kuwa linahusu jamii yetu.”
Pia Soma:
The Chanzo: Vijana Zanzibar watoweka katika mazingira tatanishi. Wazazi, polisi watoa kauli kinzani