Katika kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) kati ya Mlandege FC ya Zanzibar na Insurance FC ya Ethiopia, unaotarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi katika Uwanja wa New Amaan Complex kuanzia saa 10:15 jioni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amenunua tiketi zote za mchezo huo.
Hatua hiyo ya Rais Mwinyi inalenga kuwawezesha Nashabiki wote wa soka kuingia uwanjani bila malipo ili kuiunga mkono timu ya Mlandege FC katika mchezo huu muhimu. Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Ethiopia, Mlandege ilifungwa mabao 2-0, hivyo ushindi wa kishindo nyumbani ni muhimu ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya kimataifa.
Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) linatoa wito kwa mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi na mapema kesho, ili kuipa nguvu Mlandege FC. Mageti ya uwanja yatafunguliwa kuanzia saa 7:30 mchana.