Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wahitimu wa Kozi ya Usalama na Stratejia kuyatumia kwa vitendo maarifa waliyoyapata katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi ambapo alikuwa mgeni Rasmi. Kulingana na Mamlaka aliyokabidhiwa na sheria iliyoanzisha Chuo hicho, alitamka kuunda rasmi mkusanyiko kuwa ni Mahafali ya Kumi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania.
Mara tu baada ya Mheshimiwa Mwinyi kuanzisha Mahafali hayo, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania, Meja Jenerali Ibrahimu Michael Mhona aliwatunuku wahitimu hao Tuzo ya Kifahali ya NDC wahitimu waliofuzu mafunzo yaliyoendeshwa kwa kipindi cha majuma 47 na kufaulu kwa viwango vinavyokubalika kimataifa.
Akiwahutubia Wahitimu pamoja na wageni waalikwa, Mheshimiwa rais Dr. Hussein A. Mwinyi amebainisha kuwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kimekuwa kikipokea Washiriki ambao ni Maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Egypt, Nigeria, nchi za Commonwealth kama Bangladesh na viongozi wengine wa ngazi za juu, kutoka Wizara, Taasisi na Idara za Serikali zote mbili wamekuwa wakipata fursa ya kujiunga na Chuo hiki kwa kozi ndefu na viongozi wa Serikali kwa kozi fupi.
Source : Ulinzi Channel
NDC | Chuo cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania - Mwanzo
Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilianzishwa mwaka 2011, NDC ndicho chuo kikuu cha mafunzo ya kimkakati na taasisi kuu ya mafunzo ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. | Chuo cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania - Mwanzo