Rais Mwinyi azindua masumbwi Zanzibar, baada ya kuziwa kwa zaidi ya nusu karne

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Ulingo huu hapa Mao Tse Tung, yeas miaka mingi ya bila boxing tangu izuiwe na Abeid Karume, leo kwa mara ya kwanza tunaenda kushuhudia masumbwi. Ibra class Mawe na Mandonga, watakuwepo. Fuatana na mimi kupata yanayoendelea huko.

Ikiwa pambano linaendelea, Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi ameingia katika Uwanja wa Mao Tse Tung kuangalia mashindano hayo ambayo yanachezwa kwa mara ya kwanza August 27, 2023 baada ya kuzuiwa tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 ambapo Rais Karume aliona michezo hiyo haina tija.

Uwanjani hapo tayari mabondia walikuwa wameshapanda, hata hivyo ilibidi wakatishe pambano kupisha ujio wa rais. Mabondia walisitisha pambano kumpisha rais ni mabondia wa Zanzibar ambao wote lilikuwa ni pambano lao la kwanza.

Pamoja na Rais Mwinyi, wengine waliohudhuria uzinduzi wa mchezo wa ngumi Zanzibar ni Waziri na Naibu waziri wa Habari Zanzibar, pia naibu waziri wa Michezo Tanzania (Mwana FA).

Aliyosema Rais Mwinyi,

Serikali ilijiridhisha kuwa wadau wamekuwa wakihitaji mchezo huu wa ngumi. Hivyo serikali imeruhusu mchezo huu kwa kuzingatia sheria za kimataifa za ngumi. Mchezo huu haufanyi mabondia kuwa mahasimu ndio maana unaanza kwa mabondia kushikana mikono.

Kupitia mchezo huu, vijana wa Zanzibar wanaweza kunufaika kwa fursa zilizoko katika mchezo huu. Mchezo huu hauwanufaishi mabondia pekee bali wadau wote wanahusika na mchezo ikiwemo mapromota. Kupitia mchezo huu tunaweza kuitangaza Zanzibar.

Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya michezo hapa Zanzibar ikiwemo kuboresha viwanja, na kujenga viwanja vya kisasa kila wilaya. Zanzibar ina fursa nyingi za michezo, hivyo nawakaribisha wawekezaji wa michezo kuanzisha vitu mbalimbali ikiwemo sports academy.

Kupitia mchezo wa ngumi, tutatoa mabondia bora wa ndani na wa nje ya nchi, ambao ni muhimu katika
kukuza utalii wa nchi
1693152988048.png

Mapambano ya leo:

1. Ally Cheda Vs
Wote ni mapambano yao ya kwanza.
Pambano lilisimamishwa round ya kwanza kumpisha Rais Mwinyi
Mshindi ni .... kwa Knock Out.

2. Sebastian Cosmas Vs Masoud Khatib
Matokeo: Technical Draw

3. Hassan Salum Vs Ali Mkojani
Round 6
Mshindi: Hassan Salum

4. Said Ismail Hamad Vs Abdallah Suleiman
Round 4
Mshindi ni Said Ismail Hamad

5. Karim Mandonga Vs Othman Kiluwa
Rounds 6
Mshindi: Othman Kiluwa

6. Abdallah Pazi(Dullah Mbabe) Vs Mussa Banja
Mshindi: Abdallah Pazi, kwa KO round ya kwanza

7. Khamis Muay Thai Vs Ibra Class Mawe
Rounds 8
Mshindi; Ibrahim Class, kwa TKO baada ya Muay Thai kusalimu amri round ya 7
 
Sasa huyu ali kibakuli(ali kiba) tamasha la ngumi kuna simba kuna yanga.. ye anaimba ngoma ya simba anthem🤣🤣, unajiuliza hili tamasha la simba?

Naongea hivi mimi kama shabiki wa simba, najiuliza tu, vipi kama ningekuwepo uwanjani akaja mtu akapiga goma la yanga, najua ningekereka.
 
Utaratibu ni mbovu kweli kweli watu wameshapanda ulingoni, wapo ndani ya round ya pili, raisi ndio anaingia wao wanasimama kupigana, hotuba na vitu vingine vinaendelea.
 
Kilichozuia hapo mwanzo miaka yote ni kipi?
 
Ulingo huu hapa Mao Tse Tung, yeas miaka mingi ya bila boxing tangu izuiwe na Abeid Karume, leo kwa mara ya kwanza tunaenda kushuhudia masumbwi. Ibra class Mawe na Mandonga, watakuwepo. Fuatana na mimi kupata yanayoendelea huko.

Ikiwa pambano linaendelea, Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi ameingia katika Uwanja wa Mao Tse Tung kuangalia mashindano hayo ambayo yanachezwa kwa mara ya kwanza August 27, 2023 baada ya kuzuiwa tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 ambapo Rais Karume aliona michezo hiyo haina tija.

Uwanjani hapo tayari mabondia walikuwa wameshapanda, hata hivyo ilibidi wakatishe pambano kupisha ujio wa rais. Mabondia walisitisha pambano kumpisha rais ni mabondia wa Zanzibar ambao wote lilikuwa ni pambano lao la kwanza.

Pamoja na Rais Mwinyi, wengine waliohudhuria uzinduzi wa mchezo wa ngumi Zanzibar ni Waziri na Naibu waziri wa Habari Zanzibar, pia naibu waziri wa Michezo Tanzania (Mwana FA).

Aliyosema Rais Mwinyi,

Serikali ilijiridhisha kuwa wadau wamekuwa wakihitaji mchezo huu wa ngumi. Hivyo serikali imeruhusu mchezo huu kwa kuzingatia sheria za kimataifa za ngumi. Mchezo huu haufanyi mabondia kuwa mahasimu ndio maana unaanza kwa mabondia kushikana mikono.

Kupitia mchezo huu, vijana wa Zanzibar wanaweza kunufaika kwa fursa zilizoko katika mchezo huu. Mchezo huu hauwanufaishi mabondia pekee bali wadau wote wanahusika na mchezo ikiwemo mapromota. Kupitia mchezo huu tunaweza kuitangaza Zanzibar.

Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya michezo hapa Zanzibar ikiwemo kuboresha viwanja, na kujenga viwanja vya kisasa kila wilaya. Zanzibar ina fursa nyingi za michezo, hivyo nawakaribisha wawekezaji wa michezo kuanzisha vitu mbalimbali ikiwemo sports academy.

Kupitia mchezo wa ngumi, tutatoa mabondia bora wa ndani na wa nje ya nchi, ambao ni muhimu katika
kukuza utalii wa nchi
View attachment 2730642

Mapambano ya leo:

1. Ally Cheda Vs
Wote ni mapambano yao ya kwanza.
Pambano lilisimamishwa round ya kwanza kumpisha Rais Mwinyi
Mshindi ni .... kwa Knock Out.

2. Sebastian Cosmas Vs Masoud Khatib
Matokeo: Technical Draw

3. Hassan Salum Vs Ali Mkojani
Round 6
Mshindi: Hassan Salum

4. Said Ismail Hamad Vs Abdallah Suleiman
Round 4
Mshindi ni Said Ismail Hamad

5. Karim Mandonga Vs Othman Kiluwa
Rounds 6
Mshindi: Othman Kiluwa

6. Abdallah Pazi(Dullah Mbabe) Vs Mussa Banja
Mshindi: Abdallah Pazi, kwa KO round ya kwanza

7. Khamis Muay Thai Vs Ibra Class Mawe
Rounds 8
Mshindi; Ibrahim Class, kwa TKO baada ya Muay Thai kusalimu amri round ya 7
Safi sana
 
Back
Top Bottom