Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi jana Jumatatu alizindua tamasha la Sanaa na Utamaduni la Afrika lijulikanalo kwa jina la Festac Africa 2022, na kuzitaka serikali za Afrika kuhimiza Sanaa na Utamaduni ndani ya bara hilo.
Rais Mwinyi alisema tamasha hilo ambalo limeleta pamoja zaidi ya wasanii 10,000 kutoka Afrika nzima, linapaswa kutumika kama chombo cha kuhimiza ushirikiano na biashara miongoni mwa nchi za Afrika. Amebainisha kuwa tamasha hili ambalo linaunganisha tamaduni za Afrika limekuja kwa wakati muafaka na ni muhimu kwa juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na mamlaka za Zanzibar ili kufufua na kutangaza utalii baada ya kuathirika na janga la UVIKO-19. Amewaalika washiriki kujifunza historia, Sanaa na utamaduni wa Zanzibar na kuwa mabalozi kwenye nchi zao na pia kuitangaza Zanzibar kama kituo cha utalii.
Abdulrazak Gurnah, mshindi wa tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 2021, ni miongoni mwa wasanii maarufu waliohudhuria tamasha hilo, ambalo litaonesha Sanaa, utamaduni, urithi, muziki, utalii, sekta ya huduma na usafiri, miongoni mwa nyingine.