Pre GE2025 Rais Mwinyi: UVCCM endeleeni kuhamasisha vijana CCM ishinde na kushika dola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Mwinyi.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) ameisisitiza UVCCM kuendeleza kasi ya uhamasishaji uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha litakapoanza kwa upande wa Unguja hivi karibuni.

Ametoa wito kwa vijana kutobaki nyuma siku ya kupiga kura ili CCM ipate ushindi wa kihistoria na kuendelea kushika Dola.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Bweni la Vijana wa Kiume wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ni lazima Chama nacho kiache alama ya uongozi itakayokumbukwa kwa muda mrefu kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo na miradi ya Chama katika ngazi zote.

Halikadhalika Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa alama iliyoachwa na Serikali katika Sekta zote za Maendeleo ni lazima pia iachwe ndani ya CCM.

Vilevile Dkt.Mwinyi ameipongeza UVCCM kwa kufanikiwa kujenga Jengo hilo litakalotumika kwa harakati mbalimbali za Jumuiya hiyo.

Kwa upande mwingine Dkt.Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga Mkono juhudi za Jumuiya hiyo kwa hali na Mali ili dhamira ya kuwajenga vijana kuwa wazalendo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ifanikiwe.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa,Mohammed Ali Kawaida amesema Kauli ya Mitano Tenani kwa ajili ya viongozi wawili tu ndani ya CCM ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,Ndugu Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar, Ndugu Hussein Ali Mwinyi.
 
Tukivaa sare tunafanana - lkn hatufanani
# Vijana bodaboda - gharama za leseni viko juu
# Vijana walohitimu bado ni moto
 
RAIS MWINYI: UVCCM ENDELEENI KUHAMASISHA VIJANA CCM ISHINDE NA KUSHIKA DOLA.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) ameisisitiza UVCCM kuendeleza kasi ya uhamasishaji uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha litakapoanza kwa upande wa Unguja hivi karibuni.

Ametoa wito kwa vijana kutobaki nyuma siku ya kupiga kura ili CCM ipate ushindi wa kihistoria na kuendelea kushika Dola.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Bweni la Vijana wa Kiume wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ni lazima Chama nacho kiache alama ya uongozi itakayokumbukwa kwa muda mrefu kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo na miradi ya Chama katika ngazi zote.

Halikadhalika Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa alama iliyoachwa na Serikali katika Sekta zote za Maendeleo ni lazima pia iachwe ndani ya CCM.

Vilevile Dkt.Mwinyi ameipongeza UVCCM kwa kufanikiwa kujenga Jengo hilo litakalotumika kwa harakati mbalimbali za Jumuiya hiyo.
Kwa upande mwingine Dkt.Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga Mkono juhudi za Jumuiya hiyo kwa hali na Mali ili dhamira ya kuwajenga vijana kuwa wazalendo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ifanikiwe.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa,Mohammed Ali Kawaida amesema Kauli ya Mitano Tenani kwa ajili ya viongozi wawili tu ndani ya CCM ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,Ndugu Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar, Ndugu Hussein Ali Mwinyi.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.05.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.05.jpeg
    194.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.03.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.03.jpeg
    272.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.02.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.02.jpeg
    109.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.09.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.09.jpeg
    173.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.10.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.10.jpeg
    198 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.11.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.11.jpeg
    135.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.11 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.11 (1).jpeg
    143.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.12.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.12.jpeg
    156.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.13.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-17 at 17.23.13.jpeg
    122 KB · Views: 1
Vijana tunaangamia kwa kukosa maarifa.

CCM ipo kwaajili ya maslahi ya matumbo yao, familia zao na koo zao na sio kwaajili ya maslahi ya taifa hili na wananchi wake.
 
UVCCM ikiendeleeni kuhamasisha vijana ili CCM ishinde na kushika dola itapata faida Gani?
 
Vijana tunaangamia kwa kukosa maarifa.

CCM ipo kwaajili ya maslahi ya matumbo yao, familia zao na koo zao na sio kwaajili ya maslahi ya taifa hili na wananchi wake.
Hiyo Taasisi ni kama haipo, inajitokeza katika matukio ila kiuhalisia mitaani hakuna hao vijana.
Hamasa hakuna, wapo ktk madaftari ili kuhadaa Viongozi wa juu.
Ngazi ya Shina na Kata ni sifuri kabisa, haina mguso kwa Vijana hata kidogo na wengine wala hawaijui kama ipo.
 
Back
Top Bottom