Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya biashara kwa uadilifu, huruma na kuacha tabia ya kupandisha bei bidhaa kwakuwa wanaoumia ni wananchi.
Alhaj Dkt. Mwinyi ametoa tamko hilo leo, Ijumaa Februari 7,2025 alipozungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Jibril Mkunazini alipojumuika katika Swala ya Ijumaa.
"Hakikisheni hampandishi bei za bidhaa kwani mnawapa mzigo mzito wananchi wa kutomudu kununua bidhaa hizo muhimu," amesema Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.