Rais Mwinyi: Wafanyabishara hakikisheni hampandishi bei za bidhaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya biashara kwa uadilifu, huruma na kuacha tabia ya kupandisha bei bidhaa kwakuwa wanaoumia ni wananchi.

Alhaj Dkt. Mwinyi ametoa tamko hilo leo, Ijumaa Februari 7,2025 alipozungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Jibril Mkunazini alipojumuika katika Swala ya Ijumaa.

"Hakikisheni hampandishi bei za bidhaa kwani mnawapa mzigo mzito wananchi wa kutomudu kununua bidhaa hizo muhimu," amesema Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Your browser is not able to display this video.
 
Ni tamko la kila mwaka,
na bado bei ya bidhaa itabadirika.
 
mbona wao wanapandisha makodi kila siku zinavyokwenda? Hopeless kabisa
 
Mfungo unaanza lini shekhe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…