Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
Dada yangu Rais Samia Suluhu Hassan alisema "Rais huwa hakosei". Kwa usemi huo tu tayari alikuwa kakosea maana hakuna mtu asiyekosea, hayupo na hatakuwepo!
Ndio maana hata kwenye uteuzi wake analazimika kurekebisha, hususan baada ya kukosea uhakiki makini (vetting). Hata bunge la bajeti alilikosea mara kadhaa kwa kuliita bunge la katiba. Akasema: "sijui nina maradhi gani na katiba."
Kwa kuuacha mchakato wa "katiba mpya na nzuri" ndiyo maradhi yenyewe - kakosea sana! Huwezi kuimarisha uchumi mzuri kwa katiba mbaya na mbovu. Utazingua tu au utazinguliwa!
Miundo imara na mifumo bora ya uongozi na utawala ni kichocheo kikuu cha siasa thabiti na uchumi imara. Miundo na mifumo kama hiyo inawekwa kwenye katiba. Aidha, uhitaji wa katiba mpya na bora si utashi wa rais, bali matakwa ya wananchi, hata wasioujua umuhimu wake.
Kakosea sana! Naamini ni muungwana na msikivu, kwahiyo namwomba atengue msimamo wake na kuanza mchakato wa katiba mpya na bora kwa ajili ya uchumi imara na thabiti.
Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app