Ibrahimeliza
Member
- Nov 25, 2020
- 37
- 26
Kiongozi ni mtu yeyote ambayae anaweza na anawajibika kuongoza, mtu yeyote anaweza akawa kiongozi hata bila kuchaguliwa uongozi ni jukumu la kila mtu ni jukumu la baba kwa familia yake👨👩👧👦 na nijukumu la mama kwa familia 👨👩👧yake hata watoto pia ni viongozi wajao, kwani wanaandaliwa tangu utotoni mwao jinsi gani ya kuwa baba bora na mama bora kwa taswira hii maana yake watu wote kama sio wengi tumeandaliwa kuwa viongozi, ila kuwa kiongozi bora sasa ndomaamuzi ya mtu binafsi.
Habari nzuri ni kwamba sio lazima uzaliwe na kipaji chakuwa kiongozi, unaweza ukajifunza✍ na kuwa kiongozi bora na mkubwa ambaye utakuja kuacha alama, uongozi unafundishika kama masomo ✍mengine kama udaktari, uwalimu au uandishi wa habari, kwani haujui kama kuna masomo ya uongozi...??
Kila nyanja, kila sehemu lazima utakutana na uongozi serikalini, kwenye makampuni, biashara, shuleni🏩, msikitini🕋, kanisani💒. Yani kila sehemu kuna uongozi tofauti ni mfumo, utaratibu na namna ya kuongoza.
Wewe ni kiongozi, yule ni kiongozi na mimi pia ni kiongozi, maamuzi yapo kwenye mikono yetu.
TAHADHARI.
Kuwa kiongozi bora katika darasa lako haimaanishi ndoutakuwa kiongozi mkubwa au, kuwa kiongozi katika familia yako haimaanishi ndoutakuwa kiongozi bora katika ukoo mzima, ama kuwa kiongozi wa ukoo wako haimaanishi ndoutakuwa kiongozi wa jamii nzima, au kuwa kiongozi katika mkoa haimaanishi uwe kiongozi wa nchi.
Simaanishi kukuvunja moyo hapa, namaanisha uwe tayari, uongozi sio kitu kigumu ila pia sio kitu kirahisi, upo tayari kuwa mtatuzi wa changamoto....?? Upo tayari sifa wapate watu wengine...?? Upo tayari kulaumiwa...?? Haijalishi unaongoza nini, iwe familia, serikali, biashara au taasisi yoyote. Upo tayari........??
KIONGOZI NI KAMA UKUTA.
Ndiyo bwana kiongozi ni kama ukuta, fikiria hili kwa makini, ukuta ni matofali yaliyo pangiliwa vizuri, ikatumika saruji kushikanisha hayo matofali baada ya hapo ukaupiga lipu (plaster) ukuta wako, lipu ambayo ni mchanganyiko wa saruji(cement), mchanga na maji, ukishamaliza kupiga lipu utaupaka rangi ukuta wako ili uonekane mzuri na wakuvutia.
Kwanini kiongozi kama ukuta? Ili uwe kiongozi lazima ujenge ukuta ambao ukikaa juu ya huo ukuta utakusaidia kuona mbali, maana yake kiongozi lazima uwe na uwezo wa kifikra na kuona mbali🧠, lakini matofali hayawezi kukaa bila ya mchanga ulio changanywa nasaruji na maji, maana yake ili uwe na ukuta imara ili uwe kuongozi bora na imara, lazima uwe kama mchanga(imara)💪, saruji(busara)🤔 na maji(mnyumbulifu) kisha utapaka rangi, rangi ambayo ni uwezo na ushawishi kwa watu ili kuvutiwa na wewe kama kiongozi🧕, lakini pia ukuta hauwezi kusimama bila nguzo hapa namaanisha watu watakao kushauri katika kila hatua, viongozi wote kuanzia chini mpaka juu katika kila nyanja ni muhimu ukiusaidia ukuta wako kwakuuwekea nguzo ili husianguke.
Moja ya sababu inayomfanya mtu awe kiongozi imara,mkubwa na mwenye kupendwa na kuheshimiwa na watu ni jinsi gani anavyoweza kumudu changamoto na kutatua changamoto, mawazo mapya makubwa na mazuri katika kuisaidia jamii yake, hatutajua unauwezo kiasi gani kama kiongozi hisipokuwa kwa namna unavyoweza kutatua changamoto za jamii na kuonesha njia ya wapi tunapoelekea.
Fikiria hili, fikiria kwa makini wewe ni baba au mama katika familia ni kiongozi wewe, sio? Ndiyo, kama mkeo au mmeo hana tatizo anakupenda anakuheshimu anakujali wewe na familia yako mna watoto wanafanya vizuri shuleni, kazini au biashara zinakwenda, utaona unabahati iliyoje? Mungu kakubariki kiasi gani...?? Utajionaje nafuraha? Unaweza ukaonekana mwema, mzuri na una msimamo kiasi gani?
Haya fikiria na hili mkeo au mmeo hajatulia anavishwakwambi njee, watoto wenu wahuni, shule watoro hawana tabia nzuri, kazi au biashara ngumu haziendi, Hapo ndotutakapo jua kama kiongozi wa familia unabusara? Unaweza kumudu changamoto? Shida unazikabili vipi? Kupitia ugumu ndotunawajua hata waliotuzunguka tabia zao halisi. Kitu cha msingi hapa kiongozi wa kweli haijalishi anapitia magumu kiasi gani au mazuri kiasi gani, siku zote anakuwa bora.
MTAZAMO.
Kwakuwa hatuwezi kuzuia watu wanachofikiria na maono yao juu ya mambo au maisha kiujumla basi kama kiongozi lazima utarajie upande hasi katika watu (upinzani) haijalishi katika kila nyanja ya maisha lazima utapata mpinzani, muhimu awepo anakufanya husijisahau na anakuonesha madhaifu yako, yeye ndo mwalimu wako ukiwa ndani mchezo hauuoni ila wa njee anauona kwahiyo muachie ila kumbuka hasi mara hasi sawasawa na chanya(-×-=+),
Tanzania🇹🇿🇹🇿 ni nyumba moja kubwa, kila mtu anatamani kuchangia hata kwakubeba ndoo ya mchanga, wengine hata kwakubeba maji ili nyumba yetu ije kuwa nzuri, bora na imara, hatuna haja ya kushindana na watu wenye mijengo mikali ila tuijenge nyumba yetu kwa hatua ya mwisho ya uwezo wetu, tukiwa na ramani nzuri maana yake itatuongoza katika kuikamilisha nyumba yetu kwa wepesi, tukiwa na injinia mkuu mzuri maana yake ataisimamia vizuri nyumba yetu, sie wengine hata kwakubeba matofali ya kichwa tutabeba kuhakikisha nyumba ikamilike, kuna watakao pasua kokoto, Kwakuwa na injinia muadilifu nyumba yetu itaisha na kuwa nzuri na bora ila kwakuwa na injinia ambaye sio muadirifu najua nyumba itaisha tu ila kwakuwa imara na nzuri sina uhakika.
Ahsanta.✍✉💼

Upvote
1