Rais Onyesha Mfano wa Kuheshimu Mamlaka Zilizopo Kisheria ili Iwe Mfano na Faida Kwako Ukistaafu.

Rais Onyesha Mfano wa Kuheshimu Mamlaka Zilizopo Kisheria ili Iwe Mfano na Faida Kwako Ukistaafu.

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Nimesikitishwa sana na kauli iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu iliyo chini ya Jaji anayeheshimika kuhusu hukumu ya RC wa Arusha na kwamba mpaka dakika hii hujachukua hatua yeyote.
Huku ni kuonyesha dharau kwa mamlaka hiyo ambayo ipo kikatiba na chombo kikubwa cha msaada kwako katika utendaji wa kazi zako za kuhakikisha haki zinatendeka nchini.
Huyu Makonda mna nini naye? Au ana siri gani kiasi hata atuhumiweje kwenye mambo yasiyo faa awamu hii ya Tano (maana kwa uhalisia sio ya sita bali ya tano tuliyoichagua)bado itamlinda? Matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wengine wameshapelekwa jela, lakini huyu "mtoto wako kipenzi" kama alivyojiita hadharani tena mbele yako haguswi, kunani?
Tunataka mama Samia ukistaafu 2025 au 2030 upumzike na wajukuu bila kuacha makando kando yatakayo kunyima raha màana wakati huo huna mamlaka ya kumzuia kukusema.
 

Attachments

  • IMG-20240720-WA0002.jpg
    IMG-20240720-WA0002.jpg
    136.1 KB · Views: 2
  • downloadfile-2.jpg
    downloadfile-2.jpg
    83.1 KB · Views: 2
  • downloadfile-3.jpg
    downloadfile-3.jpg
    23.8 KB · Views: 2
  • IMG-20240720-WA0002.jpg
    IMG-20240720-WA0002.jpg
    136.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom