Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Raisi wa Russia Vladmir Putin mwenye umri wa miaka 66, jana alijiunga na wacheza judo na kupiga zoezi kwa saa moja bila kupumzika.
Putin mmoja wa viongozi huyu wenye nguvu duniani alijiung ana mzoezi hayo saa 3 usiku kwa saa za Russia na kucheza mchezo huo mara baada tu ya mazungumzo yake ni maraisi wa Iran Hassan Rouhani na raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan huko mjini Sochi.
Jambo moja la kufurahisha ni kwamba Putin alicheza na msichana bingwa wa Olimpiki wa mwaka 2016 aitwae Natalia Kuzyutina ambae aliweza kumwangusha Putin chini lakini sehemu ya picha hizo ikafanyiwa uchakachuaji.
Raisi Putin akimwangusha mmoja wa washiriki wa mazoezi hayo ya Judoka.
Akiongea baada ya mazoezi hayo Putin alisema mazoezi hayo ya ukweli humweka mtu katika hali nzuri ya kiakili na kiafya. Aiendelea kusema kwamba hali hiyo hukufanya kuwa mwangalifu na mazingira yanayokuzunguka na kukusaidia kuwa katika hali ya utayari.
Kuzyutina alipoanza kucheza na Putin aliweza kumshika kwa uziri sehemu ya juu kweye mabega na bila kutajaria Putin akajikuta akiangushwa.
Raisi Putin hakuonyesha kwamba amekasirishwa na kitendo hicho lakini akampbusu msichana huyo kuonyesha ametambua kwamba bnti nae ana stamina ya kutosha.
Raisi Putin na Natalia wakitafuta mbinu ya kuangushana.
Baadae raia wa Russia walitaarifiwa juu ya mazoezi hayo ya kiongozi wao na kuahikikishiwa kuwa yupo salama na yuko imara kimwili.
Raisi Putin akipumua baada ya zoezi kali na wachezaji wa timu ya Judo ya Russia.