Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kwa mara ya kwanza leo katika kipindi cha miaka mitatu kutafanyika tena kile kinachoitwa Mkutano wa Kilele wa Normandy kuhusu mzozo wa mashariki mwa Ukraine.
Mkutano huo ulioandaliwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel utawaleta pamoja Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Hii ndiyo itakayokuwa mara ya kwanza kabisa kwa Putin kukutana na Zelensky ana kwa ana. Hatua kupigwa katika mkutano huo wa kilele itategemea pakubwa kuhusiana na iwapo Urusi na Ukraine watakubaliana kuhusiana na maandilizi ya uchaguzi katika maeneo yanayozozaniwa ya wale wanaotaka kujitenga.