Rais Ruto ahaidi kusikiliza maoni ya vijana

Rais Ruto ahaidi kusikiliza maoni ya vijana

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa muda wowote kuanzia sasa. Hii limekuja baada ya Rais Ruto kukataa kusaini Muswada wa Fedha na kuurudisha Bungeni. Usikae mbali kufuatilia updates zaidi


Ruto atoa salamu za pole kwa waandamaji wote waliopoteza maisha katika maandamano hayo na kusema kwa waliotenda hivyo watawajibika kwa makosa yao.

Rais Ruto amesama baada ya maandamano hayo na kupokea maoni juu ya muswada huu, ameamua kutosaini Muswada Huu, na kuitaka Kenya kama taifa kuungana pamoja kupata muafaka wa jinsi ya kwenda mbele kuleta maendeleo Kenya.

Ametengeza mipango dhabiti ya kuhakikisha vijana wanapata ajira, pamoja na maoni yao kufanyiwa kazi. Ruto ameyasema haya baada ya kuulizwa na mtangazaji serikali ina mpango gani kuhakikisha inasikiliza vijana kwa wakati ujao.

====

Pia soma: LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi
 
Jana alihutubia kwa hasira ila Leo baada ya Ramani ya Ikulu kusambaa Ruto amekubali kusalimu amri.
 
Back
Top Bottom