Rais Ruto ampendekeza Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa madarakani

Rais Ruto ampendekeza Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa madarakani

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Naibu Rais.png

Rais William Ruto amemchagua Waziri wa Usalama wa Ndani, Kithure Kindiki (52), kuwa Naibu Rais mpya baada ya Rigathi Gachagua (59), kuondolewa madarakani Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limepelekwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.

Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao Maalum kilichofanyika Ijumaa.

WASIFU WA KINDIKI
Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Usalama wa Mambo ya Ndani mwaka 2022 na sasa Naibu Rais, Profesa Kithure Kindiki alihudumu kama Seneta wa Kaunti ya Tharaka Nithi, kuanzia 2013, ambapo pia alihudumu kama Naibu Spika wa Seneti; pamoja na Kiongozi wa Wengi katika Seneti.

Akiwa Kiongozi wa Wengi katika Seneti, aliongoza ajenda ya kutunga sheria ya chama cha wengi katika Seneti.

Kindiki pia amefundisha sheria na kushikilia nyadhifa mbalimbali za utawala katika kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Moi na kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Nairobi.

Alianza taaluma yake kama Mhadhiri Msaidizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Moi punde tu baada ya kuhitimu na shahada ya kwanza ya sheria.

Kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi kama Mhadhiri baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamifu katika Sheria ya Kimataifa ambapo alipandishwa cheo haraka hadi Mkuu wa Idara ya Sheria ya Umma akiwa na umri wa miaka 33 na kisha kuwa Msimamizi Msaidizi akiwa na umri wa miaka 35.

Baadaye Kindiki alipandishwa cheo kuwa Profesa Mwandamizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Ameandika machapisho thelathini na matano yakiwemo vitabu, sura za vitabu na makala katika majarida nchini na kimataifa.

Profesa Kindiki ana Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu cha Moi, Diploma ya Uzamili ya Sheria kutoka Shule ya Sheria ya Kenya, Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M), na Shahada ya Uzamifu (Ph.D.) katika sheria ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini.

Alimwakilisha Rais Ruto katika kesi iliyomkabili katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007/2008.

Endelea kusikilizia updates!

Source: BBC News
 
Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ajaye kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua Alhamisi usiku.
1729237099546.png
Jina la Kindiki limewasilishwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura. Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa leo Ijumaa.
 
Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ajaye kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limewasilishwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.

Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa Ijumaa.
Watanzania jinsi tunavo fuatilia siasa za Kenya wakati za kwetu zimetushida hata kukemea vitendo vibaya.
 
Rais William Ruto amemchagua Waziri wa Usalama wa Ndani, Kithure Kindiki, kuwa Naibu Rais mpya baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa madarakani Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limepelekwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.

Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao Maalum kilichofanyika Ijumaa.

Endelea kusikilizia updates!

Source: BBC News
Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Kenya
 
Huyu

Rais William Ruto amemchagua Waziri wa Usalama wa Ndani, Kithure Kindiki, kuwa Naibu Rais mpya baada ya Rigathi Gachagua kuondolewa madarakani Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limepelekwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.

Spika Moses Wetang'ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao Maalum kilichofanyika Ijumaa.

Endelea kusikilizia updates!

Source: BBC News
Si ndiye alikuwa wakili wa Ruto mahakama ya ICC?
 
Back
Top Bottom