Rais Ruto avunja kikosi kazi cha Polisi. Je, kile cha Hayati Magufuli kilishwavunjwa?

Rais Ruto avunja kikosi kazi cha Polisi. Je, kile cha Hayati Magufuli kilishwavunjwa?

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Jana Ruto alisema wazi kwamba ameagiza kikosi kazi cha Police kivunjwa kwa kile alichosema kilihusika kwenye kuteka na kuua watu.

Kwanini kimevunjwa?

Kumekuwa na tuhuma kwamba polisi wamekuwa wakihusika na vifo na kupotea kiholela kwa Wakenya ambapo wanaharakati wa haki za binadamu wametaka uchunguzi ufanyike.

Mnamo Aprili na Mei 2019, Shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch ilihoji watu 35 wakiwemo mashahidi, wanafamilia wa waathiriwa, madaktari na wafanyakazi wa kijamii, wanaharakati, na wafanyakazi wa polisi akiwemo msemaji wa polisi jijini Nairobi.

Shirika hilo katika ripoti yake linasema lilifanya kazi kwa karibu na mashirika washirika huko Dandora na Mathare jijini Nairobi katika kutambua waathiriwa na familia.

Mfanyabiashara ambaye pia ni mtoaji habari wa polisi aliiambia Shirika hilo kwamba polisi wana orodha ya watu wanaopanga kuwaua, wakiwemo wezi mbali na wanaume na wanawake ambao wametofautiana na maafisa hao.

Human Rights Watch pia imeandika mauaji ya kiholela katika muktadha wa ghasia za uchaguzi na oparesheni za kukabiliana na ugaidi huko Nairobi na eneo la kaskazini mashariki, na pwani katika operesheni za kukabiliana na ugaidi.

Imedaiwa kwamba baadhi ya wanachama wa kitengo hicho pia walihusika katika uhalifu wa kutumia silaha katika eneo la matuu ambapo walivamia kampuni moja ya kusambaza gesi na kuiba zaidi ya ksh.370,000 miongoni mwa visa vingine chungu nzima. Maafisa hao baadaye walinyang'anywa silaha na kushtakiwa mahakamani.

JE, KILE CHA JIWE KILISHA VUNJWA?

Sio sili kulikuwa na kikosi kazi cha sili cha kuteka na kuua watu, na hatujawahi sikia kimevunjwa, au bado kinaebdelea na majukumu?
 
BADO KIPO Serikali ni ile ile na Watu ni wale wale
 
Back
Top Bottom