Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Rais wa Kenya William Ruto pamoja na Maafisa wengine wa Serikali akiwemo Naibu Rais, Makatibu wa Baraza la Mawaziri na Wabunge, wamepangiwa nyongeza ya mishahara ya hadi 14% katika kipindi cha miaka miwili ijayo kuanzia July 2023 katika mapendelezo yaliyotolewa na Tume ya Mishahara (SRC) ili kuwanusuru dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha nchini Kenya.
Iwapo pendekezo hilo litaidhinishwa, Maafisa wa Serikali watafurahia ongezeko kubwa la mishahara itakayokidhi mahitaji yao kutokana na athari za mfumuko wa bei unaoendelea nchini humo.
Mshahara wa kila mwezi wa Rais William Ruto utapanda kwa 7.1% kuanzia July 2023 hadi Ksh. 1,546,875 (Tsh. mil 26.5) kutoka Ksh. 1,443,750 (Tsh mil 24.7) kwa sasa kabla ya kuruka kwa asilimia 6.7 hadi Ksh. 1,650,000 (Tsh mil 28.3) kuanzia July 2024.
Kwa upande wa Naibu Rais Rigathi Gachagua mshahara utapanda hadi Ksh. 1,367,438 (Tsh. mil 23,4) kutoka Ksh. 1,227,188 (Tsh. mil 21) kuanzia Julai 1 2023 kabla ya kufikia Ksh. 1,402,500 (Tsh mil 24) July mwaka 2024 ikiwa ni nyongeza ya asilimia 14.3 ya mshahara wake katika kipindi cha miaka miwili.
Wabunge wakiwemo Maseneta, watapata Ksh. 741,003 (Tsh mil 12.7) na Ksh. 769,201 (Tsh. Mil 13.2) katika miaka miwili ijayo ya kifedha mtawalia kutoka Ksh 710,000 (Tsh mil 12.2) kwa sasa, ikiwakilisha nyongeza ya mishahara ya asilimia 8.3 katika kipindi hicho, kifurushi kilichorekebishwa cha mishahara kwa Wabunge na Maseneta hata hivyo hakijumuishi marupurupu ya vikao vya kamati ambayo ni kikomo cha Ksh. 120,000 (Tsh mil 2) kwa mwezi.