Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Sudan Kusini ni miongni mwa mataifa changa sana barani Afrika, hususani Afrika Mashariki, iliyopata uhuru wake tarehe 9 July 2011, kutoka Sudan.
takwimu za mwaka 2023 zinaonyesha kwamba Sudan Kusini ina jumla ya watu zaidi ya milioni 11.
Nchi hiyo yenye utitiri wa mali asili wa kipekee sana, na utajiri mwingi wa mafuta, madini, misitu, ardhi nzuri yenye rutuba kwa kilimo, maji asili tiririka, nakadhalika nakadhalika.
Shughuli kubwa za kiuchumi nchini Sudan Kusini ni pamoja na uchimbaji mafuta, uchimbaji madini, kilimo, ufugaji, biashara na shughuli nyingine mbalimbali...
hata hivyo wanainchi wa nchi hiyo changa ni maskini wa kutupwa.
Tangu uhuru wake 2011,
nchi hiyo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2013, baada ya Rais Salva Kiir kujaribu kumfuta kazi Makamu wake Dr.Riek Machari, kitendo kilichoibua mapigano ya vikosi vya ulinzi na usalama wa Rais na huyo Makamu wake..
Tangu wakati huo, nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Africa Mashariki haina utulivu.
Vita ya kuwania madaraka miongni mwa wasomi wanaokusudia kudhibiti rasilimali na utawala miongoni mwa makundi ya kikabila na kidini vimeshamiri sana katika nchi hiyo changa..
Hivi sasa, serikali inayoongozwa na Rais Salva Kiir Mayardit, ina makamu wa rais wa tano 5, na ina jumla wizara 36 na mawaziri 36 achilia mbali manaibu mawaziri..
mabadiliko ya tabia nchi, magonjwa, mafuriko, njaa, vita na ukame vimezidisha umaskini na hali ngumu zaidi ya maisha ya kutangatanga miongoni mwa wa kaazi wa nchi hiyo yenye wakazi wasio zidi milioni 12...
unadhani nini kifanyike kuepusha na kuondoa hali hizi za mateso sana kwa wananchi maskini hususani Africa Mashariki?🐒
kugawana na kupeana vyeo na madaraka ndio suluhisho na kitulizo cha vita na migawanyiko?🐒