Rais Samia aambiwe Makamu wa Rais ni Mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, au anafanya makusudi!?

Wewe ni wakili au mwanasheria? Km sio tafuta hao watu wakueleweshe ndugu mbona mbishi. Ivi we kabila gani kwanza mana niliekezwa kwani watu ukibishana nao inapotea mda tu.

View attachment 1765312
Usidhani kuwa mtu kutokuwa mwanasheria hajui sheria na katiba; sheria siyo sayansi. Ndiyo maana watu kama Abraham Lincoln, John Quincy Adams, na Andrew Jackson walikuwa wanaijua sana katiba na wala hawakusomea sheria.
 

Sidhani kama yule jamaa waliyemsaidia kutua zigo la misumari kule Tamisemi ataweza hili fupa la maajabu ya muungano au nako wamemtegea jumba bovu ili limmalize
 
Kuliko haya makash Kash hvyo visiwa tungevitwaaga Sasa rais angekuwa mmoja zanzibar ungekuwa mkoa tuu
 
Sawa je unamengine au ayajibu kwanza haya?
 
Rais wa Zanzibar hawezi kufanya jambo lolote kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Jambo ambali Makamu wa rais na Waziri mkuu wanafanya.
Umesahau kuwa alitumwa kumuwakilisha Rais kwenye mkutano wa SADC hivi karibuni ................!!
 
Zanzibar ni nchi yenye mamlaka kamili.
 
Zanzibar ndiyo Chato yake ..... Mwendazake alishajenga hiyo precedence hiyo na watu wakatetea. Malipo hi hapahap duniani!!
kweli, mama samia tetea maslahi ya nyumbani usiogope - wape haki zao wazanzibari hata kama ni kwa mlango wa nyuma..... huyu mwendazake kapola mihela kibao kawekeza kwao bila kufuata utaratibu wa kibajeti na zingine kapeka china kuficha.
 
Mama afate protocol pengine anaamini yeye ni Raisi wa Tanganyika , Mwinyi ni Raisi wa Zanzibar so Kwa pamoja ni maraisi wa Tanzania na msaidizi wao Kwa ukarbu ndo mpango
Kwingine kote mchizi yupo sawa ila aliposema PM ni senior kwa PZ nikajua itifaki ya kuunga unga hii
 
Itifaki hazitusaidii wala hazitunyimi chochote. Na haina umuhimu wa kuwa mjadala wa kitaifa kuliko uvunjwaji wa katiba uliofanywa kuwapeleka VM-19 bungeni wasiokuwa na udhamini wa chama cha siasa.
 
Hv?makamo waraisi amechaguliwa nanani?na mh Hossein mwinyi amechaguliwa nanani hebutuanzie hapokwanza
 
You have nailed it!
 
Mkuu ungefafanua kidogo unaposema wanaishi kama yatima,wakati hawa jamaa wanamiliki biashara za maana tu huku bara na huko visiwani bila bughuda yoyote.

Sasa inahusiana nini mzanzibar/mpemba kumiliki biashara bongo! Kwani wote wanaoishi znz wana hali nzuri!!!!! Ni heri muungano uvunjwe hauna maana.
 
Bwana we. Acha liende. Katiba "in the toilet".
 

Kwa ushauri wa Nyerere? Inamaana nyinyi mnawapangia wazanzibari kwenye muungano? Hivi article of union inasemaje? In fact Muungano mshauvunja ilio baki ni kinadharia cha Ccm , hakuna makubaliano ya muungano yalio zaa Tanzania, muungano ulizaa Jamuhuri za muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Tuanzie hapo

Yes , Nani alie ondoa title ya Rais wa Zanzibar kutokuwa makamo wa Rais wa Muungano? Wakati kuna procedure zake ambazo Zanzibar na Baraza la wakilishi lazima waridhie, jee mkataba wa Muungano unasemaje Kwani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…