Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Sijua kama Raisi Samia alitafakari kina cha maneno aliyotamka akiwa huko Songea, pale aliposema Watanzania twapaswa kuwakataa wale wanaotaka kutugawa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi.
Mtu yeyote mwenye kutafakari sana ataona kama kuna wanasiasa ambao wamefanikiwa sana kutugawa Watanzania, basi ni CCM ndio waliofanya hivyo, na wanazidi kufanya hivyo. Huko nyuma, katika tawala za Mwinyi, Mkapa na hata Kikwete kwa kiasi fulani, kuwa mwanachama wa CCM au chama cha upinzani haikuwa tatizo, lakini mambo yalibadilika sana kuanzia utawala wa Magufuli na Samia, na Samia amekuwa akiendeleza ubaguzi huu wa kisiasa baada ya kuonekana kama anaanza vizuri mwanzoni.
Kila mtu anajua, wakati wa Raisi Magufuli, na Samia akiwa makamu wake, wanachama wa vyama vya upinzani walionekana kama maadui. Hata katika matukio ya kijamii, uongozi wa CCM haukutaka kabisa kuwapa ushirikiano na lilikuwa kosa kwa kiongozi wa CCM kumtembelea mgonjwa wa chama cha upinzani, au kiongozi yeyote wa CCM kutoa ushirikiano kwa viongozi wa upinzani. Na sasa hatimaye Raisi Samia anaonekana ameshawishiwa na viongozi wake wa CCM kufuata nyayo za Magufuli ikiwa anataka CCM waendelee kubaki madarakani, na sasa amebadilika na kusababisha mgawanyiko na chuki ambayo haishii kwenye mgawanyiko wa kisiasa tu bali kwenye Uzanzibar na Utanganyika.
Pia soma: Rais Samia: Tusikubali kugawanywa kwa sababu za kisiasa
Katika maeneo yenye wabunge wa upinzani, CCM wameonyesha wazi kwamba uongozi wao hautayapa kipaombele katika kuwapa huduma na fedha za maendeleo. Mkoa wa Mbeya ukiwa chini ya mbunge Sugu ulitengwa na serikali waziwazi, na umeanza kupewa mafungu ya miradi baada ya Tulia kumuondoa Sugu kwenye kiti cha Ubunge.
Mara nyingi viongozi wa CCM bila aibu wamesema ukitaka mambo yako yafanikiwe lazima uwe upande wa CCM. Hata mawaziri, wakuu wa Polisi, nk, wametoa matamko kuonyesha CCM inavyohujumu vyama vya upinzani. Na hata mifumo ya Mahakama na Polisi nchini, CCM wamehakikisha inatoa upendeleo kwa wale walio upande wa CCM zaidi ya wale walio upande wa vyama vya upinzani. Viongozi wa vyama vya upinzani wanapohamia CCM wanapewa majukwaa wawatukane na kuwakebehi viongozi wa upinzani na vyama vyao, na hata kuambiwa maneno ya kusema katika majukwaa ya CCM.
Kuhusu vyombo vya dola, CCM wamevifanya kuwa watumishi wao binafisi au watumishi wa CCM na sio serikali, iwe Polisi, Usalama wa Taifa na hata wanajaribu kuwarubuni Jeshi la Wananchi (JW), kuwafanya wawaone watu wa vyama vya upinzani ni maadui ndani ya nchi wao wenyewe Tanzania! Wamekuwa wakivijanza propaganda vyombo hivi kiasi kwamba sasa imefikia vinapotumwa kwenda kufanya kazi dhidi ya watu wa upinzani, ni kama wanapelekwa kupambana na maadui toka nje ya Tanzania!
Huko Bungeni ndio kubaya hata zaidi. Spika Tulia ameufanya Uspika kama nafasi ya kazi ndani ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM Raisi Samia, na wajibu wake ni kwa wabunge wa CCM na sio wabunge wote. Amefanya kila jitihada kuwabeza na kuwakandamiza wabunge wachache wa upinzani walio Bungeni.
Sasa Raisi Samia, acha tukuambie ukweli. Wewe na kundi lako la CCM ndio mnaotugawa sana Watanzania kwa sababu za kisiasa na tofauti za kidini. Na mbaya zaidi, mnasababisha mgawanyiko huu uende hadi kwenye Uzanzibarri na Utanganyika na kuukuza siku hadi siku. Kama kuna watu wa kutowakubali hapa nchini, basi ni nyie watu wa CCM. Mnaipeleka nchi hii sehemu mbaya sana huku mkijidanganya na nyimbo za Tanzania ni nchi ya amani! Shame on all of you!!!