Rais Samia achangia shilingi milioni kumi mfuko wa yatima na wajane mkoa wa Dodoma

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ACHANGIA SHILINGI MILIONI KUMI MFUKO WA YATIMA NA WAJANE MKOA WA DODOMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amechangia shilingi milioni kumi katika mfuko wa kuwahudumia mayatima na wajane mkoa wa Dodoma.

Mchango wake huo umewasilishwa kwa niaba yake na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika dua maalum, mashindsno ya Qur'an na iftari iliyoandaliwa Jumapili 03 April 2022 katika ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma.

Ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan tokea kuweko madarakani.

Pamoja na mchango huo amekabidhi chakula na mahitaji vituo vya watoto yatima na wajane katika wilaya za mkoa wa Dodoma.

#RamadhanMubarak
#KaziIendelee







 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…