Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

Rais Samia afanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Angellah Kairuki aenda TAMISEMI, Balozi Mulamula atemwa, Bashungwa ahamishwa

spyboss

Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
45
Reaction score
69
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Kama ifuatavyo:

Amemteua Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe. Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, Mhe. Tax anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali Mhe. Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mawaziri wote hao walioteuliwa wataapishwa tarehe 03 Oktoba, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dares Salaam.

IMG_5745.jpg
 
Bahati nzuri siku hizi hata kwenye mitihani ya darasa la pili hauwezi kuta swali waziri wa elimu anaitwa nani..?

Maana wanajua fika siku ya kuandaa mitihani na majibu, plus siku ya kufanya mtihani unakuta mawaziri wawili wametolewa na amekuja mwingine hata hafahamiki alikuwa wapi au katokea wapi!!.
 
Hivi mbunge akiteuliwa si anatakiwa kula kwanza kiapo cha ubunge?

Halafu, hadi sasa idadi ya wabunge wa kuteuliwa imefikia ngapi? Ukijumlisha wale wa JPM + 19 (Halima mdee et al)

Je, Mulamula anaendelea kuwa mbunge na kupokea posho za ubunge au anarudi kwenye nafasi yake ya hapo awali kabla ya uteuzi?
 
Back
Top Bottom