beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema mazungumzo kati yake na Rais Paul Kagame yamejikita zaidi katika kuimarisha na kukuza uhusiano wa kiuchumi.
Amesema, "Kubwa tulilokubaliana ni kukuza ushirikiano zaidi. Tanzania na Rwanda tuko kwenye Biashara na Uwekezaji, bado tuna fursa nyingi tunazoweza kutumia".
Ameongeza, "Leo tumesaini makubaliano kwamba tunaendelea kuweka uhusiano mkubwa kwenye matumizi ya TEHAMA. Rwanda mpo mbele yetu na tupo tayari kuja kujifunza kwenu".
Rais Paul Kagame amesema Taifa hilo lipo tayari kufanya kazi kwa karibu na Tanzania ili kuharakisha kufufua Mataifa hayo na Ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla kufuatia mlipuko wa janga la COVID-19
Kagame amesema changamoto zinazoukabili Ukanda wa Afrika Mashariki zinaweza kutatuliwa kwa mshikamano na fursa zinazonufaisha pande zote
Rais Samia Suluhu Hassan yupo Nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili