Rais Samia agusia ishu ya Maslahi kwa wachezaji wa ndani, Mgogoro wa Feitoto na Simba kucheza Fainali za CAF

Smart AJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
5,564
Reaction score
5,884
Leo kuna mengi Rais aliongea ila kwenye hotuba yake aligusia machache ambayo nimeya note.

1. Ishu ya maslahi kwa wachezaji wa ndani, akisema mcheza kwao hutunzwa(hapa kuna code,ambayo hata hakutaka kukaa sana kuzungumzia sanaa). Alipita juu juu tu ila camera ilitua usoni kwa eng hersi ambaye alikuwa mdogo maskini.

2. Ishu ya bwana haji kusema Simba hajawahi kucheza finali kwenye michuano hii ya CAF, ila kwa aibu kubwa sana jamaa atakuwa anajiskia vibaya kuskia kwamba rais wa nchi anasema kuwa "Simba alishawahi kufika fainali mwaka 1993”.

3. Ishu ya rais wa TFF kuwa shabiki wa timu gani kati ya simba au coastal wana mangushi, ebwana eeh kumbe rais anajua kuwa mtu mbad karia ni mwana lunyasi lia lia, licha ya Mwana FA kumdanganya kuwa rais karia ni coastal.

4. Ishu ya ndondo cup, nadhani Shaffih Dauda atakuwa kaenjoy sana na ahadi hii, Rais kagusia kipengele muhimu sana kwani soka letu linatakiwa kuanzia huko chini.

"RAIS SAMIA:SASA VIONGOZI WA YANGA NATAKA NIWAOMBE NA MIMI OMBI MOJA, SIFURAHII KUSKIA MNA MIGOGORO NA WACHEZAJI WENU, HEBU KALIMALIZENI NA FEI TOTO".

NB: bwana Haji atakuwa ana hali mbaya sana akimuona fundi Jemedari Ikulu halafu yeye anaiangalizia kwenye banda umiza.
 
Mkuu mbona umeandika kishabiki sana. Sijaangalia hiyo event ila kwani Haji alikatazwa kuhudhulia hiyo hafla au ndio sababu alifungiwa?

NB Ombi la raisi ni amri hapo Fei toto tayari kashafunguliwa.
 
Mkuu mbona umeandika kishabiki sana. Sijaangalia hiyo event ila kwani Haji alikatazwa kuhudhulia hiyo hafla au ndio sababu alifungiwa?

NB Ombi la raisi ni amri hapo Fei toto tayari kashafunguliwa.
Sijaandika kishabiki mkuu,yote hayo nimeyaona ikulu,waulize walioangalia kama nimedanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…