MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 65
- 81
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani kufuatia kifo cha Rais Dkt John Pombe Magufuli ambaye aliacha miradi mingi mikubwa ambayo kukamilika kwake kungeiweka Tanzania katika ramani nyingine ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na Bwawa la uzalishaji umeme la Nyerere (JNHPP) mto Rufiji. Hii ilisababisha hofu kwa watanzania walio wengi kuhusu kukamilika kwa miradi hiyo.
Leo tunavyoongea Rais Samia amethibitisha kwa vitendo haikua bahati mbaya hayati Magufuli kumuamini katika nafasi ya Mgombea Mwenza na Makamu wa Rais wa Nchi yetu mpaka kuvaa viatu vya Urais wa Nchi yetu kwa mipango ya Mungu. Ameukuta mradi wa JNHPP ukiwa asilimia 35 tu yeye kaufikisha asilimia 100.
Mradi huu wa JNHPP umeanza kuzalisha umeme ambapo mpaka sasa mitambo (Turbines) 4 kati ya 9 imeshawashwa na kuingiza megawati 940 kwenye gridi ya Taifa. Mradi huu unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme na utapunguza tatizo la nishati hiyo muhimu kiuchumi na kijamii hapa nchini.
Wasomi wanaeleza kukamilika kwa mradi huu ni kielelezo cha uongozi imara wa Rais Samia na ni habari njema kwa sekta nyingi ikiwemo biashara, madini, kilimo na viwanda ambavyo wawekezaji wake wamekuwa wakilalamikia gharama kubwa za bei ya nishati ya umeme na ambao sio wa uhakika hali ambayo hupelekea kuwepo kwa gharama kubwa katika uzalishaji wa bidhaa hapa Tanzania ukilinganisha na bidhaa zinazotoka nje hivyo kushindwa katika ushindani wa soko.
Kwa sasa Tanzania inalipa dola za kimarekani senti 10.7 kwa uniti moja ya umeme kiasi ambacho ni kikubwa tofauti na nchi kama Misri inayolipa dola za kimarekani senti 4.6, Korea Kusini na China dola za kimarekani senti 8, Afrika Kusini dola za kimarekani senti 7.4, India dola za kimarekani senti 6.8, Ethiopia dola za kimarekani senti 2.4, Uingereza dola za kimarekani senti 0.15 na Marekani dola za kimarekani senti 0.12.
Kukamilika kwa mradi huu uliogharimu shilingi trilioni 6.55 kutashusha bei za umeme hapa nchini kwa kati ya asilimia 35-40 hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Hongera sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan!
#TwendeNaSamia2025
#SiasaNiMaendeleo
#HakunaKilichosimama