Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani Mwaka 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Ukumbi wa The Great Hall of the People kabla ya kuanza mazungumzo Jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.
Vilevile baada ya kikao hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping na ujumbe wake katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.