Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais Samia alipopendekezwa kuwa mgombea wa urais 2025, kuna mjumbe alisimama na kuwambia yeye na mwinyi inabidi watoke nje ili wapigiwe kura, ambako Rais Samia alijibu hawezi kutoka nje, kama ni kumchana basi wamchane hapo hapo, jambo ambalo linakiuka katiba yao.
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu, Kibajaji akiwasilisha hoja ya kumtaka Samia na Mwinyi watoke ili wajumbe waamue
Yeye kuwa pale wakati anapigiwa kura ina maana ataona wote wanaomkubali na kumkataa ili baadaye alipize kisasi. Kwa mazingira hayo watu wakapiga unafki tu kukubali wote isipokuwa wachache kama Mpina walishindwa kabisa kujizuia hisia zao!
Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Kwa hicho kilichotokea ina maana Samia anatumia ushawishi wa watu fulani kufosi kuwa mgombea urais wakati wengi hawamtaki?
Kama mnakumbuka kulikuwa na kusita sita kumpitisha kutoka kwa Jakaya akiwataka wajumbe kufikiria kuhusu sheria na katiba yao inavyosema, lakini ikabrashiwa shwa shwaa kama haijasikika watu wakapishwa!
Video Jakaya akigusia kuhusu kuzingatia sheria na kuuliza wanasheria kama wanachokifanya kipo sawa
Kuna uwezekano akatokea mwamba akachallenge maamuzi hayo kama ilivyokuwa kwa Lowassa 2015?
===
Maoni ya mdau

Kile kikao, kikatiba,(ya CCM ya 1977 toleo la Disemba 2022, ibara ya 100, kifungu cha 5 c) hakikuwa cha kumpitisha mgombea urais.
Kile kikao kilikuwa cha kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM.
Habari ya kupitisha jina la mgombea urais hata haikuwa kwenye ajenda, imelazimishwa tu, tena kwa kuvunja katiba ya CCM.