Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza Wizara ya Kilimo kuisimamia kwa ukaribu Sekta ya Ushirika ili uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi uweze kufanywa na Vyama vya Ushirika.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo katika kikao na Maafisa Ugani na wanaushirika kilichofanyika Ikulu, Chamwino.
Aidha, Rais Samia amesema Serikali ina dhamira ya kurudisha hadhi ya ushirika hususan ushirika wa mazao hivyo ametaka Ushirika uendeshwe kisasa, uwekezaji ufanywe kitaalam na ukiwa na lengo la kumnufaisha mwanaushirika moja kwa moja.