Rais Samia ameahidi kuendelea kuwapa nafasi za uongozi wanawake wengi zaidi katika serikali anayoiongoza ili kufikia lengo la 50 kwa 50

Rais Samia ameahidi kuendelea kuwapa nafasi za uongozi wanawake wengi zaidi katika serikali anayoiongoza ili kufikia lengo la 50 kwa 50

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais Samia Suluhu Hassan amesema yupo tayari kushirikiana na viongozi, taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika juhudi za kufanikisha jukumu la kuipeleka mbele Tanzania.

Amesema hayo Jumapili Mei 23, 2021 wakati aliposhiriki mkutano kwa kwa njia ya mtandao kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Viongozi Wanawake Barani Afrika (AWLN).

Mkutano huo uliitishwa na rais mstaafu wa Liberia, Ellen Sirleaf kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa uongozi na kupeana taarifa juu ya fursa mbalimbali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Taarifa hiyo imewataja viongozi wengine walioshiriki mkutano kuwa ni Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ethiopia Sahle-Work Zewde, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohamed, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Malawi Joyce Banda na Rais mstaafu wa Serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika Kati Catherine Samba-Panza.

Wengine ni rais mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, Ameena Gurib- Fakim, mwanzilishi wa AWLN Tanzania na Katibu Mkuu wa mkutano wa nne wa Wanawake duniani, Getrude Mongella, mjumbe maalum wa Afrika katika masuala ya amani na usalama, Dk Bineta Diop na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya wanawake, Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Katika maelezo yake, Rais Samia amewashukuru viongozi hao kwa majadiliano waliyoyafanya na ushauri walioutoa kwake na amewaahidi kuwa yupo tayari kushirikiana nao na pamoja na taasisi na mashirika mbalimbali.

Rais Samia pia ameahidi kuendelea kuwapa nafasi za uongozi wanawake wengi zaidi katika serikali anayoiongoza ili kufikia lengo la 50 kwa 50, kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii zikiwemo afya, maji, elimu na miundombinu kama inavyoelekezwa katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka tano.

Amesema juhudi nyingine ni kukabiliana na changamoto za mazingira zinazopunguza mvua na uzalishaji wa mazao, kuweka uwazi katika matumizi ya fedha za umma na kuongeza juhudi za kukabiliana na Covid-19 na kutoa wito kwa washirika mbalimbali wa maendeleo kuongeza ushirikiano na Tanzania.

Sirleaf amesema wana matumaini makubwa na Rais Samia na kwamba wanawake wa Afrika wanamtegemea kuwa msemaji wao na mfano wa kuigwa huku Mongella akielezea kufurahishwa kwake na kutimia kwa ndoto yake ya miaka mingi akisema alitamani kuona Tanzania inakuwa na Rais mwanamke.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni sawa. Lkn azingatie zaidi uwezo wao na siyo jinsia peke yake.
Binadamu tunaongea sana ila mwisho wa siku watu wanataka MATOKEO.

Wewe balance WANAWAKE, WALEMAVU, MIKOA, KANDA, MUUNGANO, VYAMA, VIJANA na WAZEE.

Mwishowe, watu bila kujali uliteua kina nani wanahitaji kuona MATOKEO.

Na LAWAMA na PONGEZI zinakuhusu wewe.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema yupo tayari kushirikiana na viongozi, taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika juhudi za kufanikisha jukumu la kuipeleka mbele Tanzania...
Atuwekee wenye uwezo hata kama watakuwa 100% . Hii matrix ya 50-50 imekaa ki nadharia, kisiasa zaidi lakini kuitekeleza kwa minajili ya kufikia 50/50 tuu hakuna afya kwa taifa.
 
Huyu mama ata anapoongea anaonekana tu aidha aamini kama ni Rais mwenye mamlaka kamili au amaanishi kile ambacho anaongea hyo 50/50 imewezekana wapi au nchi gani hapa Duniani kuna 50/50 ? haya mpk sasa ameshafanya teuzi ngapi hao wanawake ni wangapi? Amekuwa ni muongeaji sana kuliko vitendo
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema yupo tayari kushirikiana na viongozi, taasisi na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika juhudi za kufanikisha jukumu la kuipeleka mbele Tanzania...
Hivi ikitokea vita kule frontline ktk battle field tutapeleka jinsia 50/50 au usawa ni ktk madaraka tu!!! Watu wachaguliwe uongozi kutokana na uwezo wao na siyo dini, kabila, ukanda au jinsia. Hao waliotuletea falsafa ya usawa wa kijinsia hawana hata wabunge wa viti maalum
 
Huyu mama ata anapoongea anaonekana tu aidha aamini kama ni Rais mwenye mamlaka kamili au amaanishi kile ambacho anaongea hyo 50/50 imewezekana wapi au nchi gani hapa Duniani kuna 50/50 ? haya mpk sasa ameshafanya teuzi ngapi hao wanawake ni wangapi? Amekuwa ni muongeaji sana kuliko vitendo
Rwanda jirani yako yupo zaidi
 
Aangalie uwezo, tatizo la wamama wanapenda kuwekwa nafasi za juu kisa ni wanawake
 
Back
Top Bottom