Don Moen
JF-Expert Member
- Nov 12, 2020
- 1,636
- 3,142
Rais Samia kuna wakati anafanya kazi kama simba mwenda pole, hana makeke wala mikwara lakini kuna wakati anakwarua kweli kweli.
Alianza kwa kumwagiza Kinana kuwa awaambie tafiki wapungue barabarani.
...................
Hivi karibuni tumlisikia mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Wambura akisema analifumua jeshi la polisi kitengo cha leseni.
Kwa habari za uhakika ni kuwa hii ni amri toka kwa mkuu wa nchi.
Hadi sasa wakuu wa vitengo kadhaa wanefukuzwa kazi mmojawapo akiwa ni kigogo wa polisi Mkoani Manyara.
Wengine waliokumbwa na kadhia hii ni askari waliojineemesha kupitia utoaji leseni na kuota vitambi, hawa wametolewa na kupelekwa FFU wakipisha uchunguzi wa madudu haya.
Wakati hili likiendelea kuna Kigogo mmoja aitwaye Ibra aliyekuwa mkaguzi mkuu pale Ubungi standi na baadae stendi ya Magufuli, anahemea juu juu kwani yeye ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa pesa zote toka kwa kitengo cha leseni nchi nzina naye ndiye aliyekuwa ajisambaza mzigo kwa vigogo wa polisi kitaifa.
Mbali na hawa wa leseni pia tafiki polisi nao hawana hamu kwani hawajui hatima yao kwani imeundwa tume kuwachunguza nchi nzima.
Hata dereva akijaribu kuwapa chai kama wao wanavyoita hawapokei kwa kuogopa kamera kuwanasa.
Endapo safisha safisha hii itafanikiwa itapunguza ajali hasa kwa leseni zile za kuuziwa bila mafunzo na kuongeza ufanisi kwa trafiki polisi barabarani.
Mwisho..
Poleni vishoka mliokuwa mkila na askari polisi.