sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Rais Samia amemteua Brigedia Jenerali Yohana Ochalla Mabongo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC). Jenerali Mabeyo kwa sasa ana umri wa miaka 65, inawezekana ndiyo anastaafu na maandalizi ya mrithi wake yameanza.
Inasemwa kuwa mtu anayeshika nafasi ya CDF ni mwenye cheo cha Brigedia Jenerali, ambapo ikiwa Rais hawataki wenye vyeo hivyo kushika nafasi hiyo basi option aliyonayo ni kuwaondoa watu hao jeshini ili kumpa unafuu wa kuongoza jeshi mtu atayemteua kushika nafasi ya CDF. JPM baada ya kumteua Mabeyo inasemwa kuwa Mabeyo alipata upinzani kutoka kwa mabrigedia wengine na ndipo wakaondoshwa jeshini kwa kupewa teuzi sehemu mbalimbali ili Jenerali Mabeyo aongoze jeshi vyema.
Uteuzi wa Brigedia Mabongo inaweza kuwa ndio utekelezaji wa OPTION ya kuwaondoa watu hawa jeshini na pia inaweza kuwa ishara kuwa CDF mpya atapatikana karibuni. Ingawa sijui kama uteuzi wa huyu brigedia unamuondoa jeshini (kwa maana ya kuendelea na majukumu ya kila siku ya kijeshi) au la. Wenye uelewa na haya mambo tupeni ufafanuzi.