Pre GE2025 Rais Samia amewaomba Wakazi wa Ukonga kumshika Mbunge wa Jimbo hilo Jerry Silaa

Pre GE2025 Rais Samia amewaomba Wakazi wa Ukonga kumshika Mbunge wa Jimbo hilo Jerry Silaa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaomba Wakazi wa Ukonga kumshika Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Jerry Silaa kwakuwa ni Waziri anayefanya kazi vizuri.

Rais Samia amesema hayo leo August 01,2024 akiwa Pugu njiani kuelekea Dodoma kwa treni ya SGR.

“Nawashukuru Wakazi wa Ukonga mmenipa Kijana mzuri sana Jerry Silaa, nilianza nae kwenye Sekta ya ardhi, mmeona kazi kubwa aliyoifanya kwenye ardhi, kazi ya kuendesha clinic za kutosha kutatua kero za ardhi Tanzania, sasa kwa kazi kubwa aliyoifanya nimeona sasa nimkabidhi vyombo vya habari na propaganda zetu zote za Tanzania”

“Kwahiyo sasa Mbunge wenu yupo kwenye vyombo vya habari, kazi hizi ni kubwa Ndugu zangu inawezekana
Mbunge wenu anakaa wiki tatu nne hajaonekana lakini mjue yupo kazini kunisaidia kuijenga Tanzania, kwahiyo nawashukuru sana nakuombeni mshikeni mkono tuendelee na kazi ya maendeleo kwenye Jimbo”

Snapinsta.app_452937920_1217475816286342_1173000928422059379_n_1080.jpg
 
Miaka kumi na mitano ijayo atakuwa presidential candidate tusiuliziane atapitia chama kipi?
 
Back
Top Bottom