Pre GE2025 Rais Samia amzawadia TSh Milioni 5 aliyewaokoa Watumishi wa TRA waliovamiwa Tegeta

Pre GE2025 Rais Samia amzawadia TSh Milioni 5 aliyewaokoa Watumishi wa TRA waliovamiwa Tegeta

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkabidhi tuzo na zawadi ya Tsh. milioni 5, Mkazi wa Tegeta Jijini Dar es salaaam, John Malole ambaye aliwaokoa Watumishi wa TRA walioshambuliwa Tegeta Jijini Dar es salaam wakati wakitimiza wajibu wao baada ya kuhisiwa kuwa ni Watekaji.

IMG_2715.jpeg
Rais amekabidhi tuzo hiyo katika usiku wa tuzo za walipa kodi 2023/2024 unaoendelea usiku wa leo January 23,2025 Masaki Jijini Dar es salaam.

Soma: Hizi ndizo zawadi, misaada na michango iliyotolewa na Rais Samia tangu aingie Ikulu. Ni maandalizi ya Urais 2025?
IMG_2716.jpeg
John aliwaokoa na kuwapeleka Hospitali Amani Simbayao na Watumishi wenzake wawili wa TRA walioshambuliwa wakati wakilifuatilia gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ambalo imedaiwa liliingizwa Nchini kinyemela bila kulipa kodi stahiki za Serikali ambapo wakati wakiwa kwenye pilikapilika hizo walihisiwa kuwa ni Watekaji na kuanza kushambuliwa, ambapo baadaye Amani alifia Hospitali.

IMG_2720.jpeg
Soma, Pia;
Tegeta, Dar: Maafisa wa TRA washambuliwa na wananchi kwa mawe
Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam
Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta
 
Back
Top Bottom