Matojo Cosatta
JF-Expert Member
- Jul 28, 2017
- 234
- 390
RAIS SAMIA ANA MAMLAKA YA KUMTEUA MTENDAJI MKUU WA TANROADS.
Ndugu Mpinzire katika uzi wake hapa jamiiforums amejenga hoja nzito kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hana mamlaka ya kumteua Mtendaji Mkuu wa Tanroads na uzi huu una kichwa cha habari kifuatacho: "Executive Agencies Act No 30 inaelekeza Mtendaji Mkuu wa Tanroads kuteuliwa na Waziri wa Ujenzi na sio Rais.". Kwa heshima na taadhima, ninaomba kutofautiana na Ndugu Mpinzire.
Ni kweli kabisa kuwa mamlaka ya kumteua Mtendaji Mkuu wa Tanaroads (CEO) yapo mikononi mwa Waziri wa Ujenzi kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245 (Sheria No. 30 ya 1997) kama kilivyofanyiwa mabadiliko na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Mabadiliko ya Wakala wa Serikali, 2009 yaani the Executive Agencies (Amendment) Act, 2009 (Sheria Na. 13 ya 2009) kama alivyojenga hoja Ndugu Mpinzire. Hatahivyo, ni muhimu kujua kuwa sheria za nchi ambazo zimetungwa na Bunge lazima zisomeke kwa pamoja (read in tandem) na Katiba ya nchi.
Masharti ya Kifungu cha 9 cha Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245 ( the Executive Agencies Act, Cap. 245) yanakinzana na masharti ya Ibara ya 36 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Wakati Kifungu cha 9 cha Sheria ya Wakala wa serikali, Sura ya 254 kinaelekeza kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads atateuliwa na Waziri ambaye taasisi au idara husika hiko chini ya Wizara yake huku Ibara ya 36 (2) ya Katiba inaelekeza kuwa mamlaka ya kuteua Watendaji Wakuu wa Idara na taasisi za Serikali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yako mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Masharti ya Ibara ya 36 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 yamenukuliwa neno kwa neno hapa chini kama ifuatavyo;
"36 (2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuzi unaofanywa na Rais." [Msisitizo ni wangu]
Ni Kunga (principle) ya Sheria bayana (it is a settled principle of law) kwamba iwapo sheria iliyotungwa na Bunge yaani Sheria Kuu (principal legislation) inakinzana na Katiba basi sheria iliyotungwa na bunge itakuwa batili tangia mwanzo (null et void ab initio) kwa kiwango ambacho inakinzana na katiba ya nchi, hii ni kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 64 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama yalivyotafsiriwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Kukutia Ole Pumbun & Another Vs Attorney General & Another [1993] TLR 159 , baina ya nyingine (among others).
Hivyo basi, masharti ya Kifungu cha 9 cha Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 254 ni batili tangia mwanzo ( null et void ab initio) kwa kuwa yanakinzana na masharti ya Ibara ya 36 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Kwa kuwa masharti ya Kifungu cha 9 cha Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 254 ni batili tangia mwanzo basi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana mamlaka ya kuwateua Watendaji Wakuu wa Idara na Taasisi za Serikali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mtendaji Mkuu wa Tanroads chini ya masharti ya Ibara ya 36 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
Hivyobasi, maoni ya Ndugu Mpinzire sio sahihi kwa kuwa yameshindwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 36 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. The provisions of laws enacted by Parliament (principal legislation) should not be read in partial or total isolation of the provisions of the Constitution of United Republic of Tanzania in lieu thereof the laws enacted by Parliament should be read in tandem with the Constitution.
Imeandikwa na Matojo M. Cosatta.