Pre GE2025 Rais Samia anachafuliwa na wezi na vibaka bila kujua

Pre GE2025 Rais Samia anachafuliwa na wezi na vibaka bila kujua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

NANCA

Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
92
Reaction score
100
Jamani naomba niulize hivi ni wapi ambapo ni mjini ambapo Kuna taasisi za serikali na makazi ya watu na usafiri na uwepo wa taasisi za kifedha ambapo unaweza kufidiwa square mita moja kwa Tsh. 306? Yaani namaanisha hivi ni wapi ambapo ni makao makuu ya wilaya tena upo karibu na ofisi za halmashauri ambapo wanakuja wanaojiita Serikali na wanataka kukufidia squre mita 1 ya ardhi yako kwa Tsh. 306? Swali hili naomba nijibiwe na Rais, Makam wa rais, Waziri mkuu, Waziri wa tamisemi, waziri wa ardhi na kamishina wa ardhi mkoa wa Geita.

Na katika majibu yao waniambie ni lini wataacha kuonea wananchi au lini wataacha kutumika kuonea wananchi maana huwenda tunawalalamikia wao kumbe wao nao wanatumika na viongozi wasio na akili, mambumbu na wenye historia za ujambazi na uonevu wenye kuchongea wenzao kwa wakubwa ili watumbuliwe.

Mimi Kama mimi siamini kua ni serikali ndio inayofanya ujinga Kama ule bali ni baadhi ya wanaounda hiyo Serikali kwa maslahi yao wenyewe wameamua kuisingizia Serikali wakiamini sisi na mambumbu na waoga hasa tukisikia neno serikali, kiufupi hapa serikali inatumika Kama chambo.
 
Back
Top Bottom