Rais Samia anafahamu yanayoendelea?

Rais Samia anafahamu yanayoendelea?

Burure

Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
42
Reaction score
96
Katika kipindi hichi kuelekea uchaguzi mkuu tumeona visa vya utekaji vikizidi kuongezeka siku hadi siku na tunaona mamlaka zinazotakiwa kufanya uchunguzi zikitoa taarifa kuwa zinaendelea na uchuguzi siku hadi siku

Swali langu kwa wananchi wa Tanzania na wapiga kura je, kiongozi wetu wa Nchi anajua kinachoendelea maana sijawahi ona akitoa matamko ya kukemea au kuonesha kama anafuatilia haya masuala kwani niliona akitoa millioni 30 kwenye matibabu ya Edgar (Sativa) na hakutoa statement yoyote kukemea zaidi ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii pia, alitoa milioni 5 kama rambirambi kwenye Msiba wa Ali Kibao.

Licha ya mtoto wake kutoa matamko kadhaa kuzitaka mamlaka ziwapatie taarifa ya kinachoendelea lakini bado hakuna jipya zaidi ya ukimya ukitawala kwa mamlaka husika

Je, hii Ina maana gani kwa Taifa letu na itaendelea hivi hadi lini?

Ningependa kuona raia wetu namba moja akitoka hadharani na akikemea kama alivyosema katika ajali ya Kariakoo.
Wako Mtiifu,
Katika ujenzi wa Taifa,
Burure.
 
Inawezekana hata wao sio wake
kwa hiyo ni mwendo wa hujuma tu.
 
Back
Top Bottom