Pre GE2025 Rais Samia ananishangaza anaposema CCM haina makundi

Pre GE2025 Rais Samia ananishangaza anaposema CCM haina makundi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Chama cha siasa kwa ujuzi na uzoefu niliyo nayo kinapigiwa kura na wananchi kwa itikadi sera yake na ilani yake yenye msingi wa itikadi na sera zake.

CCM ni chama cha kijamaa na kadri miaka ilivyoenda kimerekebisha namna ya utekelezaji wa mipango yake kuhusu namna ya kufikia uchumi wa kijamaa.

Mwanzo kilianza kutumia mfumo wa dola kuendesha uchumi na baada ya kushuhudia upungufu uliyojitokeza sasa kina himiza uwekezaji binafsi kwa kusimamiwa na serikali yake ili kuleta maendeleo kwa umma wa wananchi huku serikali ikibakia kusimamia zile nguzo kuu za uchumi ili kulinda uhuru wa taifa.

Pamoja na maelezo hayo kumekua na upungufu mkubwa kusimama kwenye kwenye msingi wa itikadi yake hadi chama leo kimeshikwa na mabwanyenye wasiokua na habari kabisa kwamba CCM inatakiwa kupeleka wapi taifa kiuchumu.

Hapo sasa ndio anatokea mama kuwashangaza wana CCM asilia kusema hana kundi kwenye chama.

Sasa kuna viongozi hata ukiwauliza itikadi ya CCM hawawezi kukwambia ni nini.

Watu wenye malengo binafsi ya kujitajirisha na famlia zao tu ndio wamejaa wanaongoza chama.

Tulitarajia japo mama awe anaweka kwenye uongozi wale wenye uzalendo na bado wanaamini kwenye kuleta maandeleo kwa umma wa wananch ila kuna vingozi ngazi ya juu chamani na serikalini wananekana wazi ni vibaraka wa ubeberu wa kimataifa.
 
"Tunamshukuru Mama kwa kutokuwa na Timu"
 
CCM ni kundi Moja tu 🐒

Linaongozwa na kiongozi moja pekee nae ni Comrade, Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Back
Top Bottom