GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Rais Samia
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya siku sita mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Akitoa taarifa ya ziara ya Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema ziara hiyo itaanza Agosti 2- 7 mwaka huu.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa huyo, katika ziara hiyo, Rais Samia anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya mkoa ikiwemo ya ujenzi vituo vya afya,kilimo na viwanda.
Chanzo: azamtvtz
Haiwezekani Mkoa ambao uko Jirani na Dar es Salaam miaka nenda rudi hauna Maendeleo na uko vile vile tu. Nyumba nyingi maeneo ya Mjini bado ni za Udongo na Chakavu, Miundombinu inatia Aibu ila Kutwa tu Wakazi wa Mkoa wanapishana tu Milimani kwenda kwa Waganga Kurogana.
Nina Uchungu na huu Mkoa kwakuwa ni Mkoa ambao Ukoo wangu Mmoja umelowea hapo na Kuota Mizizi yake pia.
Cc: Mdogo wangu wa damu kabisa steveachi
PIA SOMA
- Rais Samia kufanya ziara Morogoro kuanzia Julai 7, 2021
UPDATE
- Ziara ya Rais Samia Agosti 1, 2024 yasimamisha shuguli za kiuchumi jijini Dar es Salaam