Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia kuuziwa wananchi nyumba za Magomeni Kota kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi kwa kurejesha gharama za ujenzi pekee bila gharama za ardhi.
Rais Samia kasema wakitoza ardhi wahusika watashindwa kuzinunua. Pia Rais amesema wanaweza kuanza kulipa sasa polepole itakuwa vizuri ili kuwawezesha TBA kumalizia sehemu iliyobakia.
Awali waziri na msemaji wa Magomeni Kota walimkumbusha Rais Samia juu ya ahadi ya Serikali kuwa waliahidiwa kuuziwa nyumba husika kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi.
Mbunifu wa majengo na mtendaji mkuu TBA, Daud Kondoro amesema ujenzi ulianza Oktoba 1, 2016 kufuatia maelekezo ya Serikali yaliyotolewa Septemba ambapo iliazimia kujenga nyumba kwa wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika nyumba za awali. Zimetumika jumla ya bilioni 52.19 kama gharama za ujenzi.
Eneo la Magomeni Kota lina viwanja vitatu vyenye jumla ya hekta 12.9 sawa na ekari 32 ambapo TBA pia imetumia vyanzo vyake vya mapato kujenga soko kwa wakazi wa eneo hilo ambapo imejenga Magomeni Kota Machinga centre kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo pia inaendelea kujenga Magomeni Kota shopping centre.
Mwaka 2016 Rais Magufuli alifuta hati za Magomeni kota na kuhitimisha ugomvi wa miaka mingi suluhusho likiwa wakazi kuzinunua kwa bei nafuu ya jengo baada ya Serikali kumaliza ujenzi, pia kutolipa kodi miaka mitano wakati wakilipa deni.
Pia, Soma=> DAR: Rais Magufuli afuta hati na mikataba yote ya ardhi ya Magomeni Kota