Rais Samia asante sana, shikilia hapo hapo

Rais Samia asante sana, shikilia hapo hapo

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
Kwa mara ya kwanza jana (tar.17/07/21) nilipata joto halisi la ongezeko la kodi katika miamala ya simu za mkononi. Niliumia sana kwani nilishindwa kutoa kiwango fulani cha pesa kwa ukosefu wa hela ya kutolea. Lakini katika tafakuri yangu, nilijikuta namsifu sana Mhe. Rais Samia kwa ujasiri wake wa kuongeza kodi hasa katika daraja la wanyonge, kwani watumiaji wengi wa miamala ya simu na mafuta ni bodaboda, mama ntiliye, machinga, wafanya biashara wadogo wadogo etc. Miamala ya matajiri kwa sehemu kubwa inafanywa kupitia benki kwa benki au benki kwa mtu binafsi, hivyo moja kwa moja hawaja pata joto la ongezko hili.

Nimemsifu Mhe. Rais Samia kwa hoja zifuatazo;
1.
Watanzania wengi bado wana ujinga na upumbavu mwingi vichwani mwao. Bado wanadhani chochote kinachotoka serikalini ni hisani na msaada kwao. Hawajui kwamba serikali ni mali yao na inabidi ifuate matakwa yao. Wapinzani hasa CHADEMA wamekuwa critics wakubwa sana kwa serikali yetu tangu miaka ya 2000, lakini wamekuwa wakiambulia matusi na kupewa majina kutoka kwa wanyonge kanakwamba wanapigania matumbo yao. Mwaka jana (2020) ulifanyika unyang'anyi wa kiuchaguzi lakini watanzania wote walikua kimya na kudhani sio jukumu lao kupigania demokrasia na uchaguzi wa kweli. Matokeo yake bungeni kuna wabunge wa kijani tu, wanapitisha kila jambo kwa maslahi yao binafsi, huku wakiwarubuni the so called wanyonge kwa vipesa vidogo. Kwa kuwa ongezeko hili la kodi linamadhara sana kwa "wanyonge", ninamsifu sana Rais Samia na kumuomba ashikilie hapo hapo mpaka akili ziwakae sawa na wajue umuhimu wa upinzani ndani ya nchi na ndani ya bunge.

2. Watanzania wengi ni watu wa matukio ya kijinga na yakipumbavu, huku vitu vya maana wakiviweka kapuni. Kwa mfano, wakati wa bunge la budget haya yote yaliyotokea sasa yalizungumzwa sana, ila watanzania ni kama wameshtuka sasa kutoka usingizini, walikalia kwenye umbea na usengenyaji tu. Walimjadili Paula na Kajala, Diamond na BET etc wakaacha kufanya mambo ya msingi. Serikali ya CCM ilitumia mwanya huo kupitisha mambo yake, na budget iliyopitishwa na bunge inakuwa sheria, huwezi kuifuta ila kwa sheria nyingine. Namsifu Mhe. Rais Samia kwa kutumia ujinga na ushamba wa waTanzania kupitisha mambo yake na selikali yake. Mpaka akili zitukae sawa ndio mtaelewa.

3. Wapinzani(CHADEMA) wamekuwa wakipigania katiba mpya kwa ajili ya Taifa letu. Lakini jamii kubwa ya wanyonge wamejipambanunua kwamba sio kipaumbele chao. Wanyonge wanasahau kwamba, chochote wanachokiona kikifanyika kinatokana na utashi wa serikali iliyoko madarakani inayowekwa na wananchi. Wanyonge wanasahau kwa katiba ya sasa hawana uwezo wa kuweka uongozi wanao utaka wao, na hawana uwezo wa kuwawajibisha viongozi kama watafanya kinyume na matarajio yao. Mathalani, wanyonge hawana uwezo wa kuwawajibisha wabunge kwa kupitisha ongezeko la kodi katika miamala ya simu na mafuta na kupunguza kodi kwenye pombe. Wanyonge hawajui kuwa, katiba mpya ingerudusha mamlaka hayo kwao.

Wanyoge wanasema, vipaumbele vyao ni maji safi, umeme, barabara, maisha bora na huduma za jamii. Wanyonge wanadai kwamba katiba mpya sio kipaumbele chao.

Natoa heko kwa mama na waziri wa fedha kwa kupunguza uchungu wa kodi kwa matajiri na kuamishia uchungu huo kwa wanyone. Naomba mshikilie hapo hapo mpaka wanyonge wajue umuhimu wa katiba mpya.

Mapendekezo:
- Napendekeza Machinga, mama ntiliye, bodaboda, wafanyabiashara wadogo etc walipe kodi moja kwa moja TRA ili waongeze wigo wa kodi na pato la taifa.
  • Napendekeza machinga wote watolewe mijini na kwenye uholela wa kibiashara ili kupanga miji yetu iwe ya kupendeze.
  • Napendekeza wanyonge wote wapewe kadi za kijani ili kuonesha uzalendo na mshikamano kwa chama na taifa letu.

Hitimisho
Mpaka pale akili zitakapotukaa sawa hasa za wanyonge, naomba serikali yetu pendwa ishikilie hapo hapo, yaani ipige kwenye mshono. Maana kuna Watanzania wanajitoa ufahamu na kudhani hii nchi haiwahusu wao, inawahusu watawala na kikundi kidogo cha watu, iko siku wataamka.

Huu mwaka naomba niudedicate kwa wanyonye tu
 
Kati ya makundi yanayoharibu hii nchi ni hili kundi linalojiita watu wa kawaida wao wanataka kutolipa kodi , wasichangie kwenye chochote kwenye hii nchi na wakiguswa kama hivi wanalalamika mi naona hizi kodi ziendelee tu
 
Kati ya makundi yanayoharibu hii nchi ni hili kundi linalojiita watu wa kawaida wao wanataka kutolipa kodi , wasichangie kwenye chochote kwenye hii nchi na wakiguswa kama hivi wanalalamika mi naona hizi kodi ziendelee tu
Hakuna anayepinga kulipa kodi.

Watu wanalalamika kuwa tozo ni kubwa sana, zipunguzwe.
 
Back
Top Bottom