Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Dkt. Samia ameweka jiwe la msingi Julai 17, 2024 Mkoani Rukwa na kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara ya Kaengesa - Seminari ambayo ni moja ya ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mnamo mwaka 2019 Mkoani humo.
Dkt. Samia amewaahidi wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga kuwa Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Kaengesa - Seminari kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Septemba, 2024.
Aidha, Dkt. Samia ametembelea Shule ya Seminari ya Kaengesa na kumuelekeza Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kutekeleza ombi la Shule hiyo la kuunganisha barabara za lami zinazozunguka Shule hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa katika Sekta ya Ujenzi Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kukamilisha miradi yote iliyoasisiwa na Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Awali akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta ameeleza kuwa barabara ya Kaengesa - Seminari inajengwa na Mkandarasi mzawa M/s Sumry Enterprises kutoka Sumbawanga kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6.2 kwa awamu mbili za ujenzi na unasimamiwa kitengo cha TECU Mkoa wa Rukwa.