Pre GE2025 Rais Samia ataka Wakurugenzi (DED) na Wakuu wa Wilaya wanaotaka kugombea kutoa taarifa mapema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine katika serikali za mitaa kutoa taarifa mapema kama wana mpango wa kugombea ubunge.

Msingi wa kauli ya Rais Samia ni kutaka nafasi zao zijazwe mapema na watu wenye sifa huku akiwaonya kutoshtukiza wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akisema watakaoshindwa kusema mapema ipo hatihati ya kukosa yote huku wale watakaotoa taarifa mapema ikiwa watashindwa ipo nafasi nyingine ya kuweza kurejeshwa tena serikalini

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Machi 11, 2025 jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) akisisitiza kuwa hakuna umuhimu wa mtu kwenda kwenye uchaguzi kwa kubahatisha bali uchaguzi ufanyike kukiwa na watu makini katika harakati hizo za uchaguzi.

Je ni lini serikali italeta mkandarasi wa finance and buiilding? - Hamis Taletale mbunge na mtunga sheria wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM, darasa la saba!

Tunategemea kwenda uchumi wa kati
 
Yeye kuwa mbunge Kuna sheria imevunjwa? Au tuna baguana kwa kigezo cha elimu?

Vile vile wewe msomi una nafasi ya kwenda kugombea maeneo hayo ambayo yana darasa la saba.
 
Ngoja nisogee kuna nafasi ya DC mmoja hivi najua anautaka ubunge, wadau punde mtasikia nimeula huko kwenye Udc niwe nafokea wananchi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine katika serikali za mitaa kutoa taarifa mapema kama wana mpango wa kugombea ubunge.

Msingi wa kauli ya Rais Samia ni kutaka nafasi zao zijazwe mapema na watu wenye sifa huku akiwaonya kutoshtukiza wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akisema watakaoshindwa kusema mapema ipo hatihati ya kukosa yote huku wale watakaotoa taarifa mapema ikiwa watashindwa ipo nafasi nyingine ya kuweza kurejeshwa tena serikalini

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Machi 11, 2025 jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) akisisitiza kuwa hakuna umuhimu wa mtu kwenda kwenye uchaguzi kwa kubahatisha bali uchaguzi ufanyike kukiwa na watu makini katika harakati hizo za uchaguzi.

1. Mwajuma Nasonde, Mkurugenzi Moshi Manispaa, Saa100 amekubipu!
 
DED

DED Mirambo Grace jipime
 
Back
Top Bottom