Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema mtu mmoja amekutwa na maambukizi ya virusi vya Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamuro mkoani Kagera.
Taarifa hiyo inakuja siku sita tangu Shirika la Afya Duniani (WHO) liweke wazi kuhusu watu wanane kufariki dunia kutokana na ugonjwa unaoshukiwa kuwa wa virusi vya Marburg mkoani humo.
Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu, Januari 20, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Rais Samia amesema Serikali ilituma timu ya wataalamu Januari 11 mwaka huu mkoani humo na kufanya uchunguzi kuhusu ugonjwa huo na katika sampuli zilizochukuliwa ni mgonjwa mmoja pekee aliyekutwa na maambukizi hayo.
“Mpaka kufikia Januari 20, 2025 sampuli 25 zilizopimwa maabara ni mgonjwa mmoja pekee amekutwa na maambukizi na hivyo kuifanya nchi kupata mlipuko huo kwa mara ya pili. Lakini mpaka sasa nchi ipo salama na hakuna mambukizi mengine yaliyobainika,” amesema Rais Samia.
Taarifa iliyochapishwa mtandaoni na WHO Januari 13, 2025 imewajulisha nchi wanachama wake na vyombo vya kusimamia Kanuni za Afya za Kimataifa (IHR) kuhusu mlipuko wa ugonjwa unaoshukiwa kuwa Marburg katika wilaya mbili za mkoa huo uliopo Kaskazini mwa Tanzania.
Pia soma:
~ WHO: Watu nane wamefariki Kagera kwa ungojwa unahisiwa kuwa ni Marburg
~ Serikali yasema inafuatilia taarifa za uwepo wa Virusi vya Marburg Mkoani Kagera