Nawatania
Senior Member
- Jul 13, 2021
- 148
- 549
Kwanza naomba niseme mimi sio mwanachama wa chama chochote lakini kama mtu huru ninao uwezo wa kuishauri serikali na Rais wetu njia bora ya kupata Katiba mpya
Kuna watu watauliza je kwanini nimeandika moja kwa moja kwa Rais?
Jibu ni moja tu kwa katiba tuliyonayo Rais ndiye kila kitu kitakachofanyika katika nchi hii ndio maana mambo yakiharibika Watanzania moja kwa moja uwa wanamshutumu Rais aliyepo madarakani.
Nikweli Watanzania wengi wanataka katiba mpya ila vile vile wapo wengine wengi wasiotaka Katiba mpya.
Kundi la kwanza wasiotaka katiba mpya wale wananchi wasio na elimu ya Uraia hawa ni kundi kubwa sana na hawana maslahi yeyote ila hawataki tu! Na ukiwauliza watakwambia hawana faida na katiba.
Kundi la pili ni baadhi ya viongozi wastaafu wa serikali na Ccm wao wanaogopa kuibuliwa kwa mambo yao mabaya yaliyopita.
Kundi la tatu ni waliopo madarakani, Ndugu zao na Rafiki zao wengi wanahisi kuna mambo wameshavuruga hivyo wanataka katiba isipatikane mapema ili wasije wakawajibika.
Haya makundi ndio kikwazo cha katiba mpya
Naomba niende kwenye hoja, Naomba ikuwapendeza wasaidizi wa Rais wafikishe mawazo yangu kwa Rais Samia.
Rais atumie njia zifuatazo ili kufanikisha katiba mpya
Moja; Kuweka kifungu kwenye katiba mpya kwamba pale tu itakapoanza kutumika, Kwa mfano tuchukulie baada ya uchaguzi 2025 watu wote waliofanya makosa yaliyokatazwa kwenye Katiba nyuma wasamehewe na kuachwa ili wawe na amani na wawe sehemu ya mchakato wa kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya sasa.
Pili; Wale wote wasio na elimu ya katiba waelimishwe kwa kutumia mitandao ya kijamii, kufuatwa mashambani na kwenye matangazo ya Radio na Television.
Tatu; Vyama vya siasa vielimishwe umuhimu na wagomea wenye uwezo wa kushindana kwenye chaguzi hivyo mtu atateuliwa kwa sababu sio mana Ccm au Chadema atateuliwa kwa sababu ana hoja ya kuleta mabadiliko baada ya yeye kuchaguliwa.
Ziwepo opinion poll kabla ya mgomea ajateuliwa na chama chake kukiwakilisha hii itapunguza hofu ya kushindwa hasa kwa chama Tawala na kupalilia Democrasia kufanya kazi yake vizuri.
Tukifanya hivi tutapata katiba mpya kabla ya 2025 na kila mtu atakuwa na amani.
View attachment 1853300

Upvote
5