Rais Samia awataka machinga walipe kodi ipasavyo

Rais Samia awataka machinga walipe kodi ipasavyo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia Suluhu Hassan ametaja mipango ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa wafanyabiashara wadogo ikiwemo kuwa na vitambulisho ambavyo vitakuwa na taarifa zote za mfanyabiashara.

Amesema ili waendelee kuboresha mazingira ya wamachinga Zaidi ni muhimu machinga walipe kodi kadiri wanavyokadiriwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato.

Pia amewaasa ya machinga kutumika na watu wenye maduka ambao huwapa bidhaa wakasambaze, hali ambayo inawafanya wenye maduka wasilipe kodi kwa kuwa maafisa wakiwapitia EFD zinakuwa hazioneshi mauzo.
 
Hii ndio tutajua nani ni mfanyabiashara na nani ni mzururaji mjini hapa. Suala la machinga kujifanya wao ndio wafanyabiashara sana kushinda sisi wengine sasa linapata majibu rasmi.

Wakilipa kodi ndio watajua kwamba biashara haitaki ujinga ujinga wa kuchanganya siasa na biashara. Wao ndio wasaliti wakubwa sana wanabebwa na mafuso kwenda kwenye mihadhara ya CCM na wanaipigia kura na kusema upinzani haufai. Hii ni sababu wakiona dezo dezo tu, unapanga biashara popote tu Sasa tulipe wote Kodi.
 
Kwa iyo wanakuja na mpango wa vitambulisho vipya tena?.. hii nchi ni ngumu sana.

Leo wanaacha machinga wajenge pale karume, rais anasema makala atafute kandarasi wajenge soko
 
"Mungu atamalizana na upumbavu wao hivi karibuni"
Mwisho wa kunukuu, na log out 🏃
 
Ni Vema na Haki na Yeye na hao wote walioko Hightable ni bora wajitafakari kuhakikisha Kodi zinazolipwa zinafanya kazi ipasavyo
 
HAKI bin HAKI sio wengine tulipe Machinga wawe freeriders.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametaja mipango ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa wafanyabiashara wadogo ikiwemo kuwa na vitambulisho ambavyo vitakuwa na taarifa zote za mfanyabiashara.

Amesema ili waendelee kuboresha mazingira ya wamachinga Zaidi ni muhimu machinga walipe kodi kadiri wanavyokadiriwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato.

Pia amewaasa ya machinga kutumika na watu wenye maduka ambao huwapa bidhaa wakasambaze, hali ambayo inawafanya wenye maduka wasilipe kodi kwa kuwa maafisa wakiwapitia EFD zinakuwa hazioneshi mauzo.
Safi Sana Rais ,tunataka Rais mkweli na sio mnafiki..

Wanatakiwa walipe Kodi hakuna free lunch wala kulia Lia
 
Back
Top Bottom