Rais Samia awatizame NEMC kwa jicho makini. Ni uchochoro wa rushwa

Rais Samia awatizame NEMC kwa jicho makini. Ni uchochoro wa rushwa

blackice2100

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2020
Posts
2,188
Reaction score
2,897
Nimeanza kwa kuwaita mara tatu na ngoja nirudie tena!

Moja ya sekta iliyojaa uozo na uzuzu ni hawa jamaa!! Sijajua na wao kama ni miongoni mwa watu wanaojiendesha kwa hasara na ni sehemu ya wale walioko kwenye orodha ya kuenguliwa!!

NEMC kiukweli Rais awatazame hawa jamaa kwa jicho lingine ni uchochoro wa rushwa na kujiamulia wanavyojiskia.

Haya siyo majungu labda nitoe mfano hai, kuna baa ambazo mmezipachika majina eti night club!! My foot!! Mfano ni huko Ifakara mkoani Morogoro kuna baa yenyewe inajiita TikTok, nyingine Lavish na nk!

Haya maeneo ni kero haswa kwa wakazi wa Ifakara haswa wakazi wa viwanja sitini ambalo ndiko ziliko hizi baa,, miziki hawana jumatatu wala jumapili na ni mpaka alfajiri saa kumi na Moja!

Kibaya zaidi ni bahasha zinawapa kiburi na NemC ninyi NemC, natamani nitoe mitusi yote ila ninyi watu ninyi!!!

Haya maeneo yako kwenye makazi na hatukatai starehe za watu lakini toeni maelekezo basi wapake rangi za kuzuia sauti kutoka nje!! Najua haya maeneo ndiko biashara zile maarufu zinafanyika na baadhi yenu msivyo na aibu ndo wateja wakubwa ila kumbukeni haya maeneo yana watoto pia!!

NemC NemC NemC Ifakara mkoani Morogoro kiukweli natamani kuona hili jukumu ni mara mia lirudi police ninyi mbaki tu na hayo mambo ya kuzoa taka na kulinda maeneo yenye vyanzo vya maji!!! Ijapokuwa hata huko ni uozo tu!!!

Eeh Rais wetu mpendwa hebu jukumu la kusimamia maeneo ya starehe lejesha kwa jeshi la police hawa NemC hapana kwa kweli

Hawa TikTok iko siku vibahasha vyao vitawatokea puani

Hapo ni Ifakara mkoani Morogoro vipi na wewe huko kwenu mdau!!!
 
Nimeanza kwa kuwaita mara tatu na ngoja nirudie tena!

Moja ya sekta iliyojaa uozo na uzuzu ni hawa jamaa!! Sijajua na wao kama ni miongoni mwa watu wanaojiendesha kwa has

Hapo ni Ifakara mkoani Morogoro vipi na wewe huko kwenu mdau!!!
Check inbox nimekutumia namba ya Deputy Director Thobias.
 
Niambie taaisis gani ya serikali ambayo hainuki rushwa?kumbuka waliambiwa wale kwa urefu wa kamba zao.
 
Nimeanza kwa kuwaita mara tatu na ngoja nirudie tena!

Moja ya sekta iliyojaa uozo na uzuzu ni hawa jamaa!! Sijajua na wao kama ni miongoni mwa watu wanaojiendesha kwa

Hapo ni Ifakara mkoani Morogoro vipi na wewe huko kwenu mdau!!!
Hawewezi hawa hata polisi ni wale wale tu bado mwezi wa 7 wandamba wamalize mavuno vigodoro kila kona miziki usiku kucha bado kanisa la urogo mashimoni miziki mtindo 1 na vilio usiku kucha
Hakuna mwenye uwezo wa kusimamia sheria hizo ilitakiwa mkuu wa wilaya ahakikishe watu wa mabaa wanatii amri lakini wapi
 
Back
Top Bottom